Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Mudhihiri Mudhihiri (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) makao makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam kuhusu bei ya mkulima ya kununulia korosho msimu wa 2012/2013 kuwa shilingi 1,200 kwa daraja la kwanza na 960 kwa daraja la pili. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa bodi ya Korosho Tanzania Theofora Nyoni.
Na. Mwanja ibadi LINDI
Wakulima wa korosho mkoani Lindi wanavidai vyama vya ushirika zaidi ya shs bilioni 10.6 zikiwa ni malipo ya pili ya mauzo ya korosho zao baada ya kulipwa malipo ya awali ya shs 600 kutokana na bei dira ya shs 1200 kwa kilo ilivyopangwa na kupitishwa na serikali msimu wa ununuzi 2012/13
Kiasi hicho cha fedha kinachodaiwa na wakulima hao ni kati ya shs bilioni 42 zilizotarajiwa kupatika kwa wakulima baada ya kuuza korosho ambazo ni kg milioni 33 zilizozalishwa msimu huu.
Kaimu Afisa ushirika mkoa wa Lindi Saidi Mnjai amesema mkoa ulifungua msimu wa ununuzi wa korosho tarehe 10 mwenzi oktoba ikiwa ni mwenzi moja baada msimu huyo kufunguliwa kitaifa kwa kwa kufuata mfumo wa stakabadhi ghalani kwa bei dira ya shs 12000 kwa kilo.
Amesema kuwa katika msimu huo mkoa ulilenga kukusanya jumla ya kilogram 35,000,000 hadi kufikia tarehe 10 mwezi march mwaka huu jumla ya kilogramu 15,556,052 za korosho zilikuwazimeuzwa kupitia utaratibu wa mnada ambapo kati ya minada 26 iliyofanyika minada 15 haikuwa na wanunuzi baada ya wanunuzi hao kutenda chini ya bei dira.