WAGUNDUZI WA KISAYANSI WATAKIWA KUGUNDUA VITU VITAKAVYOSAIDIA WANAJAMII- DK. MWERE

Watafiti na wanasayansi nchini Tanzania wametakiwa kufanya tafiti za kiungunduzi ambazo zitaleta manufaa na kusaidia jamaii ya watanzania .


Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dr. Mwele Malecela (pichani juu) wakati wa semina ya siku moja ya wagunduzi mbalimbali iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya NIMR na Shirika la Grand Challenges la nchini Canada.


Dkt. Malecela, amesema umefika wakati sasa kwa wagunduzi mbalimbali wa Kitanzania kuanza kungundua njia mbalimbali za kuweza kutatua matatizo yaliyopo katika jamii hasa katika sekta ya afya.


Semina hiyo ya siku moja ilikuwa na lengo la kuhamasisha wangunduzi sekta ya afya ambapo baadhi ya wanasayansi wagunduzi walitoa taarifa zao za awali za namna ya kukabiliana na matizo kadha hasa kwa Mama na mtoto.


Wagunduzi kadhaa waliweza kuzungumzia gunduzi zao katika semina hiyo na miongini mwa hizo ni pamoja na ile ya hali ya Utapiamlo unaofanywa na Dkt. Magreth Kagashe, kutoka Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Bianadamu Ifakara, ambayo inafanyika katika Vijiji vya Kilombero.


Ugunduzi mwingine ni wa namna ya kusafisha maji na kuyaweka katika hali salama kupitia njia ya Takasa maji, na kuyaweka tatika hali salama na ya usafi ugunduzi unaofanya na Kijakazi Mashoto na Ugunduzi mwingine ni matumizi ya Maua ya Rosella katika kukabiliana na Upungufu wa damu kwa mama na mtoto.



Dkt. Malecela amesema ya kuwa ugunduzi unaofanyika sasa na kupewa fedha na Grand Challenge ya Canada unatakiwa uwe ugunduzi utakaoleta mabadiliko na kubadili maisha ya wananchi.


“Mara nyingi wanasayansi wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali na kugundua matatizo mengi katika jamii lakini mara chache watafiti hawa wametafuta suluhisho la matatizo hayo au magonjwa katika jamii hizo, ...kwahiyo hivi sasa wanasayansi wagunduzi wa kitanzania wamefikia hatua ya kugundua vitu ambavyo vitasaidia jamii,” alisema Dkt.Malecela.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Grand Challenge Canada, Peter Singer alisema kuwa jumlya ya miradi 16 ya ugunduzi inayofanywa na wanasayansi wa kitanzania itapatiwa fedha kupitia taasisi hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Grand Challenge Canada, Peter Singer akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya semina hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya NIMR jijini Dar es Salaam leo.Wanasayansi wagunduzi mbalimbali wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya wagunduzi. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dr. Mwele Malecela na Afisa Mtendaji Mkuu wa Grand Challenge Canada, Peter Singer, wakifuatilia kwa ukaribu mazungumzo ya Wagunduzi wa Kitanzania katika Semina ya siku moja iliyofanyika  NIMR jijini Dar es Salaam leo.Mwanasayansi Mgunduzi wa kitanzania kutoka Taasisi ya utafiti wa Magonjwa Ifakara, Dkt. Magreth Kagashe, akiwasilisha taarifa yake ya ugunduzi juu ya hali ya utapiamlo na namna ya kukabiliana nao katika jamii na kuokoa vifo vya watoto chini ya miaka 5 Kilombero.Mwanasayansi Mgunduzi wa kitanzania,Emmanuel Peter, akiwasilisha taarifa yake ya ugunduzi juu ya matuzimi ya uzalishaji wa unga wa Maua ya Rosella katika kukabiliana na upungufu wa damu kwa akina mama wajawazito na watoto.Prof. Esther Mwaikambo ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Herbert Kairuku (HKMU) akiulizwa swali. Kulia ni Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambaye pia ni Mtafiti Mkuu Kiongozi, Dk. Leonard Mboera kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).Wanasayansi wagunduzi mbalimbali wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya wagunduzi. Hii ni mara ya tatu sasa kwa Wagunduzi wa kitanzania kupata fedha za kuendesha gunzi zao na hii ndio iliyo na manufaa zaidi kuliko zote.























Previous Post Next Post