KILWA YANUFAIKA NA UWEPO WA GESI ASILIA KWA KUSAIDIA ELIMU

sahihi mkatabaMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Addo Mapunda akitiliana saini na Bi Anne Devilliers,Mratibu wa Mradi wa mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya teknorojia ya kisasa (Techonoroji Enhanced Edcation) TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni ya Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya uchimbaji,usambazaji na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo.Ulega -dc kilwaMkuu wa wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega akishuhudia utiaji wa sahihi wa mkataba huo wa miaka mitatuP1130238Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Addo Mapunda akipeana mkono na Bi Anne Devilliers Mratibu wa Mradi wa mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya teknorojia ya kisasa, mara baada ya utiaji saini.
Na Ahmeid AbdulAziz

WANAFUNZI wapatao 1,580 wanaosoma Shule tisa za Sekondari, wilayani Kilwa, mkoani Lindi,watanufaika na mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya teknolojia ya kisasa TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni ya Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya uchimbaji,usambazaji na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo.
Mradi huo wa miaka mitatu,utagharimu jumla ya Sh, ya TSh.144,945,218/-zitakazotumika kujenga misingi bora ya Lugha ya
kingereza kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanzia mwaka 2013.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Adoh Mapunda,alipokuwa akitoa taarifa katika hafla fupi ya kutiliana  saini ya utekelezaji wa mpango huo.
Mapunda alisema mpango huo,utakaochukuwa takribani muda wa kipindi cha miaka mitatu, umeanza rasmi mwezi huu kwa wanafunzi wapatao 1,580 wa kidato cha kwanza kutoka Shule tisa za Sekondari zilizopo katika wilaya hiyo.
Amezitaja Sekondari zitakazonufaika na mpango huo kuwa ni,Kilwa day iliyopo mji mdogo wa masoko, Mtanga, Songosongo, Mbuyuni,
Kinjumbi,Miteja,Mingumbi,Kikanda na Sekondari ya wasichana ya Ilulu.
Mkurugenzi Mapunda alisema mafunzo hayo kwa kuanzia yatakuwa ni ya wiki sita, yameanza rasmi hivi karibuni na kwamba walimu wapatao 30 wakiwemo (12) wa kigeni (Volunteers) wakiwemo na walimu wazawa (18). “Hizi Shule tisa kila moja italazimika kutoa walimu wawili watakaopatiwa mafunzo kwa ajili ya kuendesha mpango huu katika Shule zote hizo”Alisema Mapunda.
Aidha, Mapunda alisema kupitia ufadhili wa mpango huo wa mafunzo ya kingereza,Halmashauri ya wilaya itaendesha semina/warsha kutoa stadi za kufundishia masomo hayo kwa Sekondari hizo tisa zenye walimu wapatao (71).
Mapunda alisema mafunzo hayo ni nyongeza kwa walimu wote waliopo katika Shule hizo tisa za mafunzo ya kingereza ya aina mbili,TEE-TZ itakayoendeshwa kwa ufadhili wa ubalozi wa Marekani,(RELO-Regional English Language Office kwa Sh,24,158,480/-.
Katika ufadhili wa mafunzo hayo ya TEE-TZ na RELO jumla ya
Sh,169,103,698/-ndizo zitakazotumika kwa ajili ya utekelezaji wake.
Mratibu wa mradi huo,kutoka kampuni hiyo ya Pan African Energy,Anne Devilliers, amesema lengo la mpango huo ni, kutaka kuwawezesha wanafunzi waelewe masomo yao kwa elimu ya Sekondari na kuongeza viwango vya ufaulu katika mitihani yao ya kidato cha nne.
Devilliers akasema imebainika kwamba wapo wanafunzi waliowengi
wamekuwa hawafanyi vizuri katika masomo na mitihani yao, kutokana na kutoielewa vyema Lugha ya Kingereza.
Mkuu wa wilaya hiyo ya Kilwa, Abdallah Ulega, ameipongeza kampuni ya Pan African Energy,na akasema kwamba kwa kiasi furani itasaidia
kuboresha kiwango cha elimu ndani ya wilaya hiyo,mkoa na Taifa kwa
ujumla.
Mpango huo,ulianza kwa majaribio katika wilaya ya Mafia mkoani
Pwani,mwaka 2010 na 2011,baada ya kuona mafanikio yake,ndipo uongozi wa wilaya ya Kilwa,ukaamua mpango huo kupelekwa ndani ya wilaya yao.



++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KWA VIPURI NA MATENGENEZO YA GARI LAKO USIHANGAIKE. KAHAWA AUTO SERVICE WAKO KWA AJILI YAKO. NO. 0715331019/0785105561. LINDI TANZANIA
Previous Post Next Post