WAJAWAZITO WILAYANI KILWA WAPATA VITANDA VYA UZAZI

P1150096
Na Abdulaziz Video
AKINA mama wajawazito katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, wameanza kuondokana na tatizo la kukosa vifaa wakati wa kujifungua, baada ya Halmashauri ya wilaya hiyo kununua vitanda kumi (10) vitakavyotumika kutolea huduma ya kujifungulia.
Kununuliwa kwa vitanda hivyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya
Kikwete,alilolitoa hivi Mwishoni mwa Mwaka jana alipokuwa katika ziara ya kukagua shughuli za Maendeleo zinazotekelezwa katika Mkoa huo ambapo aliigazi Halmashauri hiyo kununua kitanda baada ya kupokea kero hiyo katika Kata ya Mitole Wilayani Kilwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo,Addoh Mapunda,


P1150133Akiongea na mtandao Ameeleza kuwa kununuliwa kwa vitanda hivyo 10 ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete,alilolitoa kata ya Mitole kwa uongozi wa Halmashaurti hiyo inunue,Kitanda
kitakachotumika ili kusaidia utolewaji wa huduma kwa Akina mama
wajawazoto watakaofika kupata huduma hiyo.
Kutokana na agizo la Rais,Halmashauri ya wilaya hiyo Imenunua vitanda zaidi ili kusaidia zahanati kumi kati ya 46 zilizopo ndani ya wilaya hiyo. Zahanati zilizonufaika na mpango huo ni,Mt Kimwaga, Nandembo, Kisangi, Kimbarambara, Kibata, Ngarambe, Tingi na Kanadawale, Jimbo la Kilwa kaskazini, ambapo kwa Jimbo la Kilwa kusini ni, Rushungi,Pande na Mitole.
Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Abdallah Hamisi Ulega
alikabidhi Kitanda cha Zahanati ya Mitole ambapo wananchi walitoa kero hiyo kwa Rais Sambamba na kununuliwa kwa vitanda hivyo, Halmashauri hiyo pia imenunua seti (12) za kuzalishia ambapo kila seti moja imegharimu kiasi cha Sh,400,000/-.
Hata Addoh Mapunda, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo amesema kununuliwa kwa vitanda hivyo, sio tu ni utekelezaji wa agizo la Rais Kikwete, pia ni uendelezaji wa utekelezaji wake, kwani tayari Zahanati 36 kati ya hizo 46 zilikwisha nunuliwa vitanda vya aina hiyo na kufanya Zahanati zote kuondokana na tatizo hilo kwa sasa
Ni kweli Zahanati za Kilwa na Jiografia ya kufika Hospital ya Wilaya
au Mkoa ni Ngumu sana ila Jitihada za Idara ya Afya, Pamoja na Utawala yaani Ofisi yangu Tukishirikiana na Mkuu wa Wilaya kwa kutafuta Ufadhili Tumeanza kujidhatiti kusaidia Jamii ila Naomba Hata Madiwani Watupe Ushirikiano kwa kuwa wao kwa kushirikiana na watendaji na Wenyeviti wa Vijiji Watasaidia kushauri ili sisi Tujikite katika Uboreshaji wa Huduma kwa Karibu.Alimalizia Mapunda.
Decemba 04 mwaka jana, Rais Jakaya Kikwete, alipotembelea Shule ya Sekondari ya kata ya Mitole iliyopo wilayani Kilwa,katika risala yao
wananchi walimuomba kuwasaidia kuwapatia kitanda kwa ajili ya
kujifungulia akina mama wajawazito wakati wa kujifungua,ambapo naye aliuagiza uongozi wa Halmashauri hiyo kutekeleza hilo.



++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KWA VIPURI NA MATENGENEZO YA GARI LAKO USIHANGAIKE. KAHAWA AUTO SERVICE WAKO KWA AJILI YAKO. NO. 0715331019/0785105561. LINDI TANZANIA
Previous Post Next Post