Huu Ndio UJio Mpya wa CHIDI BEENZ

Rapper Kutoka Ilala, Rashid Makwiro a.k.a Chidi Beenz anataraji kuachia mdundo wake mwingine hivi karibuni. Chidi ambae alitamba na sana ngoma zake kama Ngoma Itambae [Dar Es salaam Stand Up], Mmenisoma, Mashaalah, Nipokee na zinginezo anataraji kuachia track hiyo ambayo amefanya na mwimbaji kutoka Tanzania House Of Talent [T.H.T], nikimzungumzia Barnaba.
Chidi aliandika, "Soon nitaachia wimbo wangu mpya nimefanya na young broda Barnaba toka ThT pamooja na sauti mbili tatu za hapa na pale kutoka kwenye nyumba ile. Mwisho"
Wow!! inaonekana Chidi alipata muda wa kutosha kutembelea nyumba ile [THT]... Haha
King Kong ambae pia ni kiongozi wa kundi la LA FAMILIA lenye maskani yake kitaa cha Ilala, ni mmoja wa wasanii wa muziki aliyefanya collabo nyingi sana na wasanii wa kizazi kipya ikiwa ni pamoja na wasanii wa taarabu na genre nyinginezo hapa nchini.
Well... Mashabiki wa Chidi Ujio Ndio Huo Kaaeni Mkao wa Kula..!


Previous Post Next Post