VIDEO YA "MACHAFUKO" YALIYOTOKEA BUNGENI LEO

Bunge limelazimika kusitisha shughuli zake hadi kesho kufuatia maamuzi ya bunge kuondoa hoja ya Mh John Mnyika juu ya uboreshaji upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika jiji la Dar es salaam ambapo kufuatia kitendo cha kuondolewa kwa hoja hiyo wabunge wa kambi ya upinzani hawakukubali na kusimama wote kwa pamoja na kuanza kuzomea na kuimba.PictureWabunge wa upinzani wakiwa wamesimama wote kwa pamoja kupinga hoja Bungeni
PictureNaibu Spika Bunge,Mh. Job Ndugai (kulia) akionyeshwa makabrasha na Mbunge wa Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassari muda mfui baada ya kuahurishwa kwa kikao cha Bunge leo.PictureMnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mh. Tundu Lissu (kulia} akijadiliana jambo na Naibu Spika wa Bunge,Mh. Job Ndugai nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.Wengine ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mh. Joshua Nassari na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa. (picha na Mwanakombo Jumaa - Maelezo.)
Previous Post Next Post