Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Mussa Azzan Zungu pamoja na wajumbe wa kamati yake wakiwauliza maswali mbalimbali Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Segerea lililopo jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo ilitembelea sehemu wanapolala Wafungwa na Mahabusu, jikoni, ghala la chakula pamoja na kuzungumza na Maafisa wa Jeshi hilo na baadaye Mahabusu na Wafungwa.Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu akizungumza na Mahabusu na Wafungwa wa Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati kamati yake ilipofanya ziara ya kikazi katika gereza hilo jana. Kamati hiyo ilitembelea sehemu wanapolala wafungwa na mahabusu, jikoni, ghala la chakula pamoja na kuzungumza na Maafisa wa Jeshi hilo na baadaye Mahabusu na Wafungwa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akiahidi kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali za Mahabusu na Wafungwa wa Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) walipozitoa kupitia hotuba yao iliyotolewa wakati Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ilipofanya ziara katika gereza hilo jana.Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, John Chiligati akizungumza na maofisa wa Jeshi la Magereza wakati kamati hiyo ilipofanya ziara katika Gereza la Mahabusu la Segerea, jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Azzan Zungu, anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi. Kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Home
»
HABARI ZA KITAIFA
» KAMATI YA BUNGE YA ULINZI NA USALAMA YAFANYA ZIARA KATIKA GEREZA LA MAHABUSU LA SEGEREA, JIJINI DAR
About Author
JE, UNA HABARI, PICHA, TANGAZO, MAKALA NA USHAURI? USISITE KUWASILIANA NASI SIMU / WHATSAPP NAMBA 0625535420.