Vinara wa ligi kuu ya vodacom na mabingwa wa Africa mashariki na kati, Yanga wanatarajia leo kucheza mchezo wao wa kwanza toka watoke Uturuki kwenye kambi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom.
Yanga watacheza na Black leopards ya Afrika kusini mchezo unao ratibiwa na Prime time promosheni, utakao chezwa katika uwanja wa taifa ukitanguliwa na mchezo kati ya Yanga Veterani na watangazaji wa Clouds fm.
Black leopards wamewasili jana jijini Dar es salaam teyari kuwavaa vinara hao wa ligi kuu ya vodacom waliopoteza michezo miwili na kutoa sare mmoja katika ziara yao ya Uturuki.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.