Na Mwandishi wetu: Ahmeid A.Azizi
MKOA wa Lindi umetajwa kuwa na viwango vikubwa vya wanawake na watoto walioathiriwa na utapi amlo (Lishe bora),hali ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia kuathiri zaidi udumavu wa urefu,ukondefu na umri kwa wananchi wa mkoa huo.
Hayo yameelezwa jana na mwakilishi kutoka Ofisi ya waziri mkuu,Liliani Mshiu,alipokuwa akifunga tamasha la kuhimiza Lishe bora,iliyofanyika uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Mshiu amesema hali ya viwango vya utapiamlo hapa nchini inaendelea kuongezeka kwa kikasi kikubwa licha ya jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuutokomeza kwake.
Mshiu akasema wanawake na watoto ndio wanaoathirika zaidi na utapiamlo ikiwemo kupata udumavu wa urefu na umri kunakochangiwa na kukosekana kwa Lishe bora.
Amesema kukosekana kwa Lishe bora uliodumu kwa kipindi kirefu, kumechangia kwa asilimia 54% kwa wananchi wake kuwa na tatizo la ukondefu,uzito na kupungua kwa urefu kutokana na kukosa lishe bora uliodumu kwa muda mrefu.
Pia amesema kutokana na kushamili kwa hali hiyo,upo uwezekano mkubwa wa vifo iwapo watapata magonjwa ya uambukizo, ukiwemo ugonjwa wa ukimwi.
Mwakilishi huyo kutokam Ofisi ya waziri mkuu amesema asilimia 77% ya wanawake na watoto wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 45, bado wanakabiliwa na milo ambayo kwa kiasi furani haikidhi mahitaji halisi ya virutubisho,na hivyo uwa na hali mbaya zaidi.
Amesema kutokana na upungufu wa wekundu wa damu kwa wanawake walio katika umri wa uzazi, ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi (bila ya kutaja takwimu zake).
Mshiu akasema kwa kutambua athari za utapiamlo katika afya na uhai wa watoto na wanawake,kumeifanya taasisi ya Chakula na Lishe,kuanzisha juhudi za kuhamasisha Jamii kuwa na mipango yenye misingi itakayoiwezesha Taifa kuwa na wananchi walio na afya njema.
Aidha akasema Shirika la Save the Children kwa kushirikiana na taasisi ya Chakula nchini (TFNC) zinatoa ushauri wa utekelezaji wa masula hayo na tafiti zinazosaidia kuboresha huduma za Lishe.
Alisema Lishe inapoimarishwa uwezekano wa kupunguza magonjwa na vifo na hivyo kufikia malengo ya millennia Namba 4 na 5 ya Lishe bora ambayo kimsingi ni muhimu kwa wanadamu wote.
Naye, kaimu mkuu wa mkoa wa Lindi, Dkt, Nassoro Hamidi kwa upande wake alisema amefarijika kuona kampeni hiyo,ni jambo muhimu sana kwa wananchi wa mkoa huo,kutokana na kutambua jitihada za Serikali,Asasi za kiraia katika kupambana na utapiamlo.
Dkt, Hamidi alisema ili kuwa na maendeleo thabiti katika juhudi hizi pamoja na kupunguza vifo vya akina mama na watoto wadogo ambayo usababisha kwa matatizo yakiwemo ya utapiamlo.
Naye,mkurugenzi wa Shirika lisiloa la kiserikali la Save the Children,Mary Msangi Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza juhudi za kuwekeza kwenye Lishe kwani ni afya kwa wanaadamu na maendeleo ya Taifa letu.
Alisema majukumu ya Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) ni kusaidiana na Serikali kueneza mikakati ya Lishe kwa Taifa katika kukuza ufahamu na utashi wa Jamii kwa kuleta mabadiliko chanya yatakayoleta Lishe bora kwa watanzania.