Unknown Unknown Author
Title: CRDB IMEIPATIA MIKOA YA LINDI &MTWARA MIKOPO YA SH,32.0 MILIONI.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
BENKI ya CRDB imeipatia vyama vikuu vya ushirika katika mikoa ya kusini, Lindi na Mtwara,jumla ya Sh,32.0 milioni kwa ajili ya ununuzi wa z...
BENKI ya CRDB imeipatia vyama vikuu vya ushirika katika mikoa ya kusini, Lindi na Mtwara,jumla ya Sh,32.0 milioni kwa ajili ya ununuzi wa zao la korosho kwa wakulima wa mikoa hiyo katika msimu wa mwaka huu.
Mwakilishi wa Benki hiyo,kutoka Jiji Dar es salaam,Elizabert Masuke,ameyaeleza hayo,alipokuwa akiwasilisha taarifa katika kikao cha wafanyabiashara na taasisi za fedha kilichofanyika mjini Kilwa Masoko,wiki iliyopita.
Akiwasilisha kwa taarifa yake hiyo,Masuke alisema tayari Benki hiyo imeshavipatia vyama vya ushirikavya mikoa ya Lindi na Mtwara,jumla ya sh,32.0 milioni, kwa ajili ya kununulia zao la korosho kwa msimu wa mwaka huu.
Pia alisema kutokuwepo kwa soko la uhakika la zao la korosho msimu wa mwaka huu na kushuka kwa minada,hususani kwa mkoa wa Pwani ni miongoni mwa sababu kwa mabenki yasite kutoa fedha zake kiholela.
Mwakilishi huyo alisema tayari kwa mwaka huu, Bodi ya CRDB wameshaidhinisha na kuipatia mikoa ya Lindi na Mtwara,jumla ya Sh,32.0 milioni.

Alisema kati ya hizo Sh, 18.0 milioni zimeidhinishwa na kutolewa kwa mkoa wa Mtwara, wakati Sh, 14.0 milioni oa wa Lindi,kwa ajili ya kununulia korosho za wakulima.
“Mh, Rais fedha nyingi kama hizi lazima Benki pekee hazina uwezo wa kupitisha hadi Boidi ikae na kuidhinisha, na tayari mikoa ya Lindi na Mtwara,wameshaidhinishiwa na tayari fedha hizo zimeshapelekwa kwenye vyama mbalimbali vya msingi”Alisema Masuke.
Mwakilishi huyo wa CRDB alisema tayari baadhi ya vyama vya msingi,bila ya kutaja majina yake,kwa mkoa wa Mtwara vimeshawalipa wakulima fedha zao, na kwamba vingine vimeanza kurejesha mikopo waliyokuwa wameichukuwa.
Kwa upande wa mkoa wa Lindi, Masuke alisema tayari Sh,9.0 milioni kati ya Sh,14.0 zilizopitishwa na Bodi ya CRDB zimeshatolewa kwa vyama husika na kutumika kununulia korosho, ikiwa ni pamoja na baadhi ya vyama kurejesha mikopo hiyo.
“Mh, Rais lazima tuseme ukweli,huku kwenye biashara yta korosho kuna ujanja ujanja mwingi,hivyo tusipokuwa makini katika utowaji wa fedha,tunaweza kujikuta hasara yote inarejea kwenye mabenki,,,,,,,na baadae kuendelea kuomba Grentee kwa Serikali” Alisema Masuke.
Naye,Salum Mkame,mwakilisha wa wafanyabiashara alisema kutonunuliwa kwa korosho za mkoa wa Pwani,kunachangiwa na wakulima wenyewe kutozingatia utaratibu wa kuzipanga korosho zao kwenye madaraja na kuzitunza vizuri kama wafanyavyo wenzao wa mikoa ya Lindi na Mtwara.
Mkeme alisema kitendo cha wakulima hao,kuchanganya korosho mzuri na mbovu,ndiko kunakosababisha kutonunuliwa kwa korosho za mkoa huo wa Pwani.
“Hivi ni mfanyabiashara gani atakayekuwa tayari kununua biashara mbovu?” Alihoji Mkame.
Alisema haiwezekani mkoa kama wa Pwani ukawa na korosho za daraja la pili pekee,na kueleza iwapo wakulima wa mkoa huo watajirekebisha kwa kuzipanga korosho zao katika madaraja yanayotakiwa upo uwezekano mkubwa wa kununuliwa kama ilivyo katika mikoa mingine inayozalisha zao hilo la korosho hapa nchini.
Naye, mwenyekiti mpya wa Chama kikuu cha mkoa wa Pwani,(Corecu) Juma Abedi alisema mkoa huo una zaidi ya tano 4,000 zipo kwenye maghara zikikosa wanunuzi,hali ambayo inawafanya wakulima wakate tama, ikiwa ni pamoja na kushindwa kwa baadhi yao kusomesha watoto wao.
Baada ya kusikiliza vilio vya pande zote hizo, Rais jakaya Kikwete,ameliagiza Bodi ya Korosho nchini, kukaa pamoja kati yao na wafanyabiashara na vyombo vya fedha kuangalia uwezekano wa kutatua tatizo hilo, ili kuweza kuwaokoa wakulima wa zao hilo mkoani Pwani na maeneo mengine.














About Author

Advertisement

 
Top