Kocha wa
timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Polusen (kulia)
akishuhudia kwa makini mchezo wa Kundi A, kati ya Uganda na Ethiopia, Kombe la
Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Kagame Uwanja wa Mandela,
Namboole, Kampala, Uganda. Wengine kushoto kwake ni Michael Mukunza wa
Executive Solutions, Waratibu wa udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa
Stars na Kocha Msaidizi, Sylvester Marsh.
Wachezaji wa Timu ya taifa ya Uganda wakishangilia goli lao la kwanza na lapekee katika Mchezo wao wa leo dhidi ya Ethiopia, hadi mwisho matokeo ni Uganda 1-0 Ethiopia
Kipa namba
moja wa Uganda, Abbel Dhaira akiwa jukwaani kufuatilia mchezo huo, kushoto ni kimwana
aliyekuwa naye. Abbel hatacheza tena mashindano haya baada ya kuumia kwenye mechi ya ufunguzi na Kenya jicho lililovimba kulia.