Unknown Unknown Author
Title: SIMBA YATWAA UBINGWA WA SUPER 8
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TIMU ya Vijana ya Simba ‘Simba B’  leo imedhihirisha ubora wake baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya kwanza ya Banc ABC Sup e r8  baada ya...
TIMU ya Vijana ya Simba ‘Simba B’  leo imedhihirisha ubora wake baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya kwanza ya Banc ABC Super8  baada ya kuibamiza Mtibwa Sugar mabao 4-3.
Katika mchezo huo wa fainali uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba ilionekana kutawala kila idara katika mchezo huo ambapo vijana hao waliwahenyesha wapinzani wao Mtibwa.
Edward  Christopher ndiye alianza kuiandikia Simba bao la kwanza katika dakika ya 12 alipoitendea haki pasi ya Haruna Athuman  na kumuuza kipa wa Mtwibwa, Shabani Kado langoni mwake.
Dakika ya 32 Shaban Kisiga aliisawazishia  Mtibwa kwa bao la mkwaju wa penalty  ambapo mwamuzi Hashim Abdallah kuamuru hivyo kutokana na mchezaji wa Simba  Omary Salum kumchezea vibaya Jamal Mnyate wa Mtibwa. Bao hilo lilidumu hadi timu hizo zinakwenda mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu kucheza kwa umakini huku   Simba wakicheza mpira wa akili na kuwachosha wakatamiwa hao wa Mtibwa na kuwafanya  kucheza mpira wa kutumia nguvu.

Christopher aliiandikia tena Simba bao la pili katika dakika ya 52, akimalizia krosi ya Rashid Ismail, kabla ya Mtibwa kusawazisha katika dakika ya 56 kupitia Kisiga aliyepiga shuti kali nje ya 18 na kumshinda kipa wa Simba.
Simba ilipachika bao la tatu katika dakika ya 66 likipachikwa na Haruna Athuman mara baada ya kuwatoka mabeki  wa Mtibwa, kabla  Hassan Seif kuitumia safi faulo na kusawasazisha katika dakika ya 73.
Dakika 90 za mchezo huo ambao ulishuhudiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Dh.Fenella Mukangara ambaye alikuwa mgeni rasmi,zilimazika kwa timu hiyo kwenda sare ya mabao 3-3 hivyo mwamuzi kuongeza dakika 30.
Alikuwa ni Christopher tena ambaye aliifungia Simba bao la ushindi katika dakina ya 102 alipomalizia kazi safi ya Frank Sekule na kufanya bao hilo lidumu hadi dakika ya 120 na kuifanya Simba kushinda kwa mabao 4-3.
Kwa ushindi huo, Simba imepata milioni 40 pamoja na medali , huku Mtibwa ikiondoka na shilingi mil 20 pamoja na medali.
Aidha, shujaa wa Simba Christopher alizawadiwa sh milioni mbili kwa kuwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao 7, huku kipa wa Simba Abuu Hashim alizawadiwa sh milioni 2.5 kwa kuwa mchezaji bora.
Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi Agosti 8 na kuzishirikisha pia timu za Simba, Mtibwa Sugar, Azam Fc,Polisi Morogoro kwa upande wa Bara, huku Visiwani iliwakilishwa na  Mafunzo ,Zimamoto, Mtende na  Super Falcon.
Simba:Abuu Hashim, William Lucian, Omary Salum, Hassan Isihaka, Hassan Hatibu, Said Ndemla, Haruna Athuman, Abdallah Seseme, Rashid Ismail, Edward Christopher na Ramadhan Singano/Fank Sekule.
Mtibwa Sugar:Shaban Kado, Malika Ndeule, Yusuf Mguya, Salum Swedy, Salvatory Ntebe, Babu Ally, Jamal Mnyate, Awadh Juma, Juma Javu, Shaban Kisiga/Hassan Seif na Vicent Barnabas.

About Author

Advertisement

 
Top