Wanahabari wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Lindi wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Bw Reubern Mfune mara baada ya kufungua mafunzo ya siku nne kwa ya kuwajengea uwezo wanahabari kuhusiana na uandishi wa Habari za Mahakamani.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Lindi, Abdulaziz Ahmeid(Channel ten)akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa ,Reubern Mfune kufungua mafunzo ya siku nne kwa wanahabari hao.
Wanahabari toka vyombo mbalimbali wakihudhuria mafunzo hayo ili kujengewa uwezo wa kuandika kwa mujibu wa sheria Habari za mahakamani
Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Bw Juma Thomas,Mwanasheria wa kujitegemea akitoa mafunzo kwa wanahabari
Wanahabari 18 wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Lindi kufuaria mradi wa "Press club" Wameanza mafunzo ya uandishi wa habari za mahakamani ikiwa ni mfululizo wa Mafunzo yanayoendeshwa na Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Tanzania
Mafunzo hayo ya siku nne yanashirikisha wanahabari toka vyombo mbalimbali yameanza jana Wilayani Ruangwa na kufunguliwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo
Baada ya mafunzo hayo Wanahabari hao watafanya mkutano mkuu wa mwaka wa klabu hiyo ikifuatiwa na Mkutano wa Wadau wa Habari walio katika wilaya hiyo
Mafunzo hayo yanayoendeshwa kwa ufadhili wa mradi wa Press Club Chini ya Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzani(UTPC)Yameanza leo wilayani Ruangwa.