WAISLAM WAOMBWA KUTOCHAGUA NYUMBA ZA IBADA WANAPOHITAJI KUOMBA NA KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU

image Mkuu wa wilaya ya Lindi,Dr Nassor Ally Hamid akifungua msikiti wa madhehebu  Ahamadiya huku  viongozi wa madhehebu hayo wakishuhudiaimage Waumini wa kiislam wa mjini Lindi wakishuhudia tukio hiloimage Mwandishi wa Mtandao huu ambae pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Lindi Abdulaziz Ahmeid akiongea na Mwasisi wa Jina la Tanzania,Bw Mohamedi Igbal Dar AMBAE ndie aliefanikisha ujenzi huo kwa kuchangia tshs Mil 50
image Kiongozi wa Ahmadiya  Nchini  Tahir Mohamedi,akitoa neno baada ya Uzinduzi wa msikiti huo
WATANZANIA wameaswa kujiepusha na vitendo vya vurugu, ili kuliepusha Taifa kuzalisha kizazi vitakavyoashiria udini na ukabila,hali itakayoweza kusababisha uvunjivu wa umoja,amani na mshikamano uliosisiwa na baba wa taifl Mwl Julius Kambarage Nyerere, Rai hiyo imetolewa jana na mwanzilishi wa jina la Taifa hili (Tanzania) Mohamedi Igbal Dar,alipokuwa anazungumza na timu ya waandishi wa habari hizi muda mfupi baada ya kikao cha ndani cha ufunguzi wa Misikiti uliojengwa mjini Lindi,kwa ufadhili wa Taasisi ya Ahmmady Iqbal alisema vitendo vya vurugu vinayoanza kushamili hivi sasa hapa nchini,visivyoangaliwa kwa umakini na kuchukuliwa hatua,vinaweza kulipeleka taifa katika katika machafuko yasiyoisha, na hivyo kuondo sifa ya Tanzania aliyoiacha mwanzishi wa taifa hili, mwalimu Nyerere miaka kumi na tatu iliyopita.
Alisema kuwa vurugu zinazojitokeza hivi sasa kwenye Shughuli mbalimbali zikiwemo za dini pamoja na siasa, ni ishara mbaya kwa nchi kama ya Tanzania,ambayo imetimiza zaidi ya miaka  50 ya uhuru wake,na kugeuzwa kuwa ni kisiwa cha amani na utulivu.
Igbal ambaye kwa sasa maisha yake yapo nchini Uingereza, alisema kuna haja ya vitendo hivyo kudhibitiwa mapema iwezekanavyo kabla havijaota mizizi ya kuatarisha amani, umoja na mshikamano uliopo wa taifa hili. Alisema kwamba vurugu sio jambo la kujivunia sana katika Taifa linahitaji kuendelea, kama la Tanzania  na kuwasisitiza  watu wasiojua
athari za  kivita vya kidini  waangalie  nchi za  jirani  kama vile Somalia  ambapo wananchi wake  wanaishi bila amani.
Nae kiongozi wa  Jumuia ya Ahmmadyya  nchini Tanzania Tahir Mohamedi, amewataka waislamu   kufuata  sheria  kanuni na makatazo ya mwenyezimungu  kupitia kwa Mtume wake Muhammad (Saw) kuungana  na kuwa kitu  kimoja  kwa kuwa dini yao,  haifundishi  waumini  wake kueneza chuki. Tahir  alisema dini zote  dunia zinafundisha  amani, huruma na upendo
miongoni mwa waumini wake watu wengine, lakini  ikiwa watu wachache wanaenda kinyume na   maagizo ya mungu  basi sio vizuri jamii kuwahukumu waislamu wote wa Tanzania.
“Unajua  mwanzilishi wa Jumuhia ya waislamu  wa Ahmmadyya ametufundisha  kuwa ikiwa  mnapenda  kupata ridhaa ya mungu  basi takaseni  mioyo yenu  kwa kuwa  haina wazo la chuki  na fanyeni uadilifu  hata kama  mbele yenu  kuna adui yenu” alisema Tahir

 






Previous Post Next Post