Unknown Unknown Author
Title: VPL KAMA KAWA, LIGI YA TAIFA KURINDIMA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ni mwisho wa juma jingine ambalo litawakutanisha tena wapenzi wa Soka la Bongo katika viwanja tofauti vya Bongo, ambapo Ligi kuu ya Vodac...
vodacom-red-logo-vodafone1
Ni mwisho wa juma jingine ambalo litawakutanisha tena wapenzi wa Soka la Bongo katika viwanja tofauti vya Bongo, ambapo Ligi kuu ya Vodacom (VPL) itakuwa inaendelea katika viwanja tofauti vya Tanzania Bara.
Katika mwisho wa juma hili kutakuwa na uanzaji wa ligi ya Taifa ngazi ya wilaya katika wilaya tofauti, ambapo Sports In Bongo ina taarifa ya kuanza kwa ligi ya wilaya ya Dodoma.
LIGI KUU YA VODACOM
AZAM KUKAA KILELENI KWA MDA
Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi watakuwa na kibarua cha kusaka ushindi wa goli 3-0 mbele ya African Lyon katika uwanja wa Azam uliopo pembezoni mwa jiji la Dar es salaam, hapo kesho (oktobar 6).
Azam FC wataitaji ushindi wa goli hizo ili kuipiku Simba SC katika msimamo wa ligi hiyo ambapo Simba SC wakicheza mchezo wao wa 6 siku inayo fuata.
Azam FC itakuwa ikicheza mchezo wake wa 5 huku ukichachiwa na urejeo kamili wa nyota wake Salum Abubakari 'Sure Boy Jr' aliyeingia kipindi cha pili katika mchezo uliopita.
Katika msimu uliopita Mzunguko wa Kwanza African Lyon ndio timu pekee iliyoifunga Azam FC katika uwanja wake wa Azam, hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na ikumbukwe kuwa African Lyon wametoka kupata ushindi dhidi ya Toto African katika mchezo wake wa mwisho na kuwa timu ya kwanza kuifunga Toto African msimu huu.

RUVU KUWA WA KWANZA KUIFUNGA COASTAL Baada ya Coastal union kucheza michezo mitano bila kupoteza, huku michezo mitatu ya ugenini wakiambulia sare, hapo kesho (oktobar 6) watakuwa na kibarua cha kuendeleza rikodi yake watakapo karibishwa na Ruvu Shooting katika uwanja wa Mabatini uliopo Pwani.
Ruvu shooting wametoka katika kupoteza michezo mitatu mfululizo miwili wakicheza jijini Dar es salaam zidi ya Simba SC, Mtibwa Sugar, huku watatu ukiwa dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wake wa Mabatini.
Ruvu shooting watakuwa wanasaka ushindi wa pili mbele ya Coastal Union ya Tanga baada ya kuwachapa Mgambo Shooting katika uwanja huo wa Mabatini ukiwa ndio ushindi pekee katika michezo 5 aliyocheza.
SIMBA KUENDELEA KUWAFUNZA WAJENZI WA TAIFA
Baada ya kupunguzwa kasi na mpinzani wake wa jadi Yanga, Mnyama Simba SC itakuwa na kibarua cha kuendelea kuwafunza soka timu za jeshi la kujenga Taifa, pale watakapo wakaribisha JKT Oljoro katika uwanja wa Taifa hapo Oktoba 7.
JKT Oljoro kama ilivyo kwa Simba SC bado hawajapoteza mchezo wowote wa ligi kuu ya Vodacom na wanakutana katika uwanja wa taifa wote wakitoka katika michezo yao ya mwisho kwa matokeo ya sare.
Simba SC ndio waliokuwa wa mwanzo kuwafunga JKT Oljoro katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom msimu uliopita na kuipotezea dira, ambapo walianza kupoteza michezo na kujikuta wakitoka nafasi ya 3 mpaka nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi.
Mshambuliaji wa Simba SC Emmanuel Okwi anatarajiwa kulejea uwanjani hapo jumapili baada ya kukosa michezo mitatu ya ligi kuu ya vodacom kwa adhabu ya kadi nyekundu.
YANGA KATIKA UWANJA WAZAMANI WA MANJINJIO
Miaka ya hivi karibuni uwanja wa Kaitaba unaotumiwa na Kagera Sugar kama uwanja wake wa nyumbani umekuwa ukipunguza makali ya kuchinja timu zinazoshuka kuwakabili wakata miwa wa Kagera.
Oktoba 7 Yanga wakiwa chini ya kocha wao Muholanzi watakuwa katika uwanja huo kusaka point 3 kutoka kwa Kagera ambayo imetoka kushinda katika mchezo wao wa mwisho ugenini.
Yanga ikishuka bila ya Kelvin Yondani aliye majeruhi na Saimon Msuva aliyezawadiwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita dhidi ya Simba SC, wanakumbukumbu ya kupoteza point 3 katika safari yake ya mwisho katika uwanja huo.
MICHEZO MINGINE YA VPL 07/10/12
MGAMBO JKT Vs POLISI MOROGORO, Mkwakwani
TOTO AFRICANS Vs JKT RUVU, CCM Kirumba
T.PRISONS Vs MTIBWA SUGAR, Sokoine
LIGI YA TAIFA NGAZI YA WILAYA
LIGI ya Taifa ngazi ya Wilaya ya Dodoma Mjini inatarajiwa kuanza keshoambapo timu 20 zitachuana kumtafuta bingwa wa Wilaya. Ligi hiyo itachezwa katika viwanja viwili tofauti.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Katibu Msaidizi wa Chama cha Soka Wilaya ya Dodoma Mjini (DUFA), Saidi Babuji alisema maandalizi yote kwa ajili ya ligi hiyo yamekamilika.
Alizitaja timu za kundi A kuwa ni Dodoma Sports, Kisasa FC, Gwasa United, Nungu FC, Saratoga, FC Hungry, Area C, Cardif FC na West Chinangali.
Timu za kundi B zimetajwa kuwa ni Dundee United, Jupiter, KBC, Area D, Kikuyu FC, Vijana Stars, Hazina, Pentagon, Area A na Ipagala FC.
Babuji alisema kuwa, kila kundi litakuwa na timu 10 na kila kundi litatoa timu tatu ambazo zitachezwa hatua ya sita bora na hatimaye bingwa wa Wilaya atawakilisha Wilaya kwenye Ligi ya Mkoa pamoja na mshindi wa pili na watatu.
Alibainisha kuwa, ligi hiyo itachezwa kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Jamhuri na kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Central.
Timu ya Kisasa na Gwassa ndizo zitakazo fungua pazia la ligi hiyo zitacheza kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi hiyo.
Alizitaka timu zote kufuata kanuni na taratibu za mchezo wasoka na hawata vumilia timu ambazo zitaonesha utovu wa nidhamu.

About Author

Advertisement

 
Top