Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania katika kukuza Uimara Na kujenga Uhuru wa Vyombo vya habari na Waandishi wa Habari unatoa mafunzo kwa kwa Waandishi na wamiliki wa vyombo hivyo Mkoani Lindi ili kuwajengea Uwezo wa kuomba Ruzuku zinazotolewa na Mfuko huo..
Mafunzo hayo ya Siku moja yanawezeshwa na Mshauri wa mambo ya Habari ambae pia ni mwandishi Mkongwe,Bw Ndimara Tegambwage na Meneja wa Vyombo vya Habari vya SJMC Chini ya Chuo kikuu cha DSM,Bi Edda Sanga.
Kufuatia awamu ya pili ya Utoaji Ruzuku hizo toka TMF, Mfuko umeamua kutoa mafunzo hayo ili kutoa msisitizo katika Uandishi wa Habari za Vijijini, Uwazi na Uwajibikaji,Utawala bora, Ukimwi, Jinsia na kuwapa sauti za jamii zilizotengwa ili waandishi waweze kupata habari kwa jamii na habari zinazogusa jamii.
Tags
Lindi