Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Rick Ross akiimba jukwaani usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake kwenye viwanja vya Lidaz Club,wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta likirindima.
Mashabiki wakitaka kuangusha uzio uliowekwa kwa ajili ya usalama.
Mkali mwingine wa miduara AT na madansa wake wakilishambulia jukwaa
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,akiimba jukwaani na shabiki wake
Msanii wa miondoko ya rusha rohoo a.k.a Miduara,Shilole akijiachia jukwaani vilivyo na madansa wake usiku huu mbele ya umati mkubwa uliofika kwenye viwanja vya Lidaz Club,katika kuhitimisha kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Watu kibao wakiwa ndani ya viwanja vya lidaz club.
Mwanamuziki kutoka nchini Marekani,Rick Ross akijisikia furahaa kuwaona Watanzania wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumshuhudia yeye akikamua stejini.