Unknown Unknown Author
Title: COASTAL WACHAPWA, AZAM WEMBE ULE ULE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Coastal Union ya Tanga leo imepoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom ikiwa ni mchezo wa pili kuwa chini ya kocha Hemedi Moroco...
Coastal Union ya Tanga leo imepoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom ikiwa ni mchezo wa pili kuwa chini ya kocha Hemedi Moroco katika uwanja wa Mabatini. Wakati Azam FC wakiendeleza wimbi lao la ushindi katika uwanja wa Azam.
COASTAL UNION YAONJA LADHA YA KUPOTEZA
Coastal union ikiwa chini ya Kocha Hemedi Moroco aliyechukuwa nafasi ya Juma Mgunda leo walikuwa wageni wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Mabatini ikiwa ni mwendelezo wa ligi kuu ya Vodacom. Katika mchezo huo ulioshuhudia kwa mara ya kwanza Coastal Uniom wakipoteza mchezo, Ruvu Shooting waliandika goli la kuongoza katika dakika ya 5 ya mchezo kupitia kwa Hussein Swedi. Haikuwa chukua mda Ruvu Shooting kufunga goli lake la pili, ambapo katika dakika 12 kipindi cha Kwanza Hassan Dilunga aliipatia goli la pili na kupelekea mchezo kumalizika kwa Ruvu Shooting kuichapa goli 2-0 Coastal Union. Huo ni ushindi wapili wa Ruvu shooting iliyoshuka uwanjani mara 6 na kupoteza michezo 4. Mchezo wao wa mwanzo kushinda walishinda dhidi ya Mgambo Shooting ya Tanga pia. Coasta Union ni mchezo wao wa pili kuwa chini ya kocha wao mpya Hemedi Moroco. Mchezo wake wa kwanza alitoa sare na JKT Oljoro jijini Arusha.
AZAM FC WAIPUMULIA SIMBA SC
Azam FC wamefanikiwa kuendeleza wimbi la ushindi na kuifikia Simba SC, huku wakishindwa kukaa kileleni kwa kufikisha point 13 sawa na vinara Simba SC wakizidiwa goli moja. Azam FC leo ilikuwa wageni wa African Lyon katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi na kufanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0. Goli la Azam FC lilipatikana katika dakika ya 45 likifungwa na mfungaji bora msimu uliopita John Raphael Bocco ambapo lilikuwa goli lake la pili msimu huu. Katika dakika ya 87 Azam FC walipata pigo baada ya beki wake wa kushoto Samih Hajji Nuhu kuzawadiwa kadi nyekundu na mwamuzi Israel Majuna Nkongo


About Author

Advertisement

 
Top