Kweli ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni. Katika kitendo cha kustaajabisha, mwanaume mmoja nchini India, alimlevya mkewe na madawa, akazitoboa kuta mbili za uke wa mkewe, na kuanzia siku hiyo, akawa akiufunga uke wa mkewe kwa kufuli kila aendapo kazini.
Inadaiwa njemba hiyo ilifanya kitendo hicho miaka minne iliyopita, na kumpa mkewe mateso, fedheha, na udhalilishaji huo wa kupigwa kufuli mara kwa mara kwa kipindi cha miaka minne.
Mwanamke huyo alijaribu kujiua kwa kutumia sumu ya panya. Zoezi hilo la kujiua lilifeli na mwanamke huyo anayeitwa Sitabai Chouhan, alikimbizwa hospitalini. Wakati manesi wakimfanyia uchunguzi, walipigwa na butwaa baada ya kugundua kufuli lililofungwa katika sehemu zake za siri.
Alipolazwa katika hospitali hiyo ya Maharaja Yashwant Raoin, uke wake ulikua bado umefungwa na kufuli. Kufuli liliweza kuondolewa baadae baada ya polisi kumsaka na kumpata mume wake, aliyewapatia ufunguo wa kufuli hilo.
Kiongozi wa polisi, Konstebo Chhaganlal(linatamkwa vipi jina hili!?) alisema “Manesi wamethibitisha kuwepo kwa kufuli hilo. Ni baada ya kumkamata mumewe na kupata ufunguo ndipo kufuli hilo liliweza kuondolewa.”
Njemba hiyo inayoitwa Sohanlal Chouhan ilisema: “Nilifanya hivyo sababu wanawake kadhaa katika familia yetu walifanya uzinzi nje ya ndoa zao muda uliopita”
Bi. Chouhan bado anaendelea na matibabu hospitalini na anategemewa kupona kikamilifu. Amesema alijaribu kujiua sababu mumewe alijaribu kumbaka binti yao wa kwanza. Wakati huo huo, mumewe amefunguliwa mashitaka ya ukatili na kusababisha maumivu ya hali ya juu.
Vitendo vya uke “kufungwa” ili kuzuia wasichana na wanawake wasifanye ngono (chastity belt) ni vitu vya kawaida nchini India lakini kawaida hutumia kipande cha nguo. Naona njemba hii ikaona kipande cha nguo hakiaminiki na kuona kufuli la kweli ndio mpango mzima, hivyo akaamua kuapgredi. Pichani chini ni mwanamke huyo akiwa hospitali, na picha ya pili ni mtuhumiwa (mumewe)