YANGA B 'WAITILIA UBANI' YANGA A TAIFA, WAPIGA MTU SITA HUKU YANGA A WAKIPIGA 3-0


Yanga B imeifunga TMK United ya Ligi Daraja la Pili, mabao 6-1 katika mchezo wa utangulizi kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Polisi Morogoro. Mabao ya Yanga yamefungwa na Georgeb Banda matatu katika dakika za 61, 70 na 72, Hussein Moshi dakika ya 12 na Rehani Rehani dakika ya 19 na 27, wakati la kufutia machozi la TMK United, lilifungwa na Abdi Hashimu dakika ya 62. Tazama picha za mechi.Mchezaji wa Yanga B akivaa jezi kuingia dakika 10 za mwisho
Mchezaji wa yanga B akimtoka beki wa TMKGeorge Banda kulia anawafunga tela mabeki wa TMK United Wachezaji wa Yanga, Mbuyu Twite, Haruna Niyonzjma, Ally Bart6hez na Nadir cannavaro wakishuhudia wadogo zao wanavyotoa adhabu, Katika Mchezo wao Yanga Wameifunga Polisi Morogoro Magoli Matatu Kwa Bila hivyo kuifanya timu hiyo kuwa nyuma ya Simba SC kwa Point Moja katika Msimamo Wa Ligi hiyo ya Vodacom Tanzania Bara.
Previous Post Next Post