Ligi Kuu ya Grand Malt Zanzibar (ZGPL) imeendelea leo katika uwanja wa Amaani ambapo walikutana Chuoni na Bandari, mchezo uliomalizika kwa Bandari kuwachapa 2-1 Chuoni. Kwa ushindi huo wa leo Bandari wamejikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Grand Malt kwa kufikisha point 13 baada ya kushinda michezo minne na kutoka sare mmoja huku wakiwa bado hawajapoteza mchezo wowote ule.
Tags
ZANZIBAR