Unknown Unknown Author
Title: Simba yaanza ligi kwa ushindi mnono
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Siku ya jumamosi ilikuwa ni ufunguzi wa michezo ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania, timu zote za Ligi kuu zilikuwa vitani. Simba sc walikuw...

Siku ya jumamosi ilikuwa ni ufunguzi wa michezo ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania, timu zote za Ligi kuu zilikuwa vitani.
Simba sc walikuwa uwanja wa taifa wakipambana na African Lyon, wameibuka na ushindi wa mabao 3-0, mabao ya Simba yakiwa yamefungwa na Emmanuel Okwi na Mrisho Ngasa.
Hadi kufikia mapumziko Simba alikuwa akiongoza kwa bao 2-0 Okwi na Ngasa wakiwa wafungaji, kipindi cha pili Simba walipata bao kwa njia ya Penati kupitia Akuffo. African Lyon nao walikosa penati katika kipindi cha kwanza, baada ya mkwaju wa Bakar kuokolewa na Juma Kaseja.
Yanga wakiwa ugenini huko Mbeya wameambulia pointi moja baada ya kutoka sare ya 0-0.
Coastal Union katika Derby yao wakitoka na ushindi wa bao 1 bila dhidi ya Mgambo.
Azam FC wameshinda ugenini bao 1 dhidi ya Kagera.





About Author

Advertisement

 
Top