Unknown Unknown Author
Title: WAKAZI WA MASASI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi Farida ….amesema zoezi la sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2012, ni muhimu na hailengi kutafuta ...
image Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi Farida ….amesema zoezi la sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2012, ni muhimu na hailengi kutafuta dini ya mtu bali ni kutafuta idadi ya Watanzania ili nchi iweze kupanga maendeleo. Bi alieleza hayo leo alipokuwa akiongea na mtandao huu wilayani humo Alisema kwa upande wa Wilaya yake ,lengo la sensa ni kutambua idadi halisi ya wakaazi wa Wilaya hiyo na Mkoa hali itakayosaidia kuharakisha uandaaji wa sera na utekelezji wa dira na mipango ya maendeleo.
Alisema zoezi la kuhesabu watu litaanza  Usiku wa Leo (Agosti 26), na kuendelea kwa siku saba ambapo kila mtu atakaelala wilayani humo na Nchini  atahesabiwa, hivyo aliwataka wananchi kutunza kumbukumbu za taarifa kwa ajili ya maswali yatakayoulizwa na makarani wa sense wataofika katika kaya na maeneo yao Alifahamisha kuwa taarifa za matokeo ya takwimu zitakazokusanywa zitabakia kuwa ni siri kwa mujibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2007 ya ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar, pamoja na sheria ya takwimu ya mwaka 2002 ya ofisi ya Taifa ya takwimu.Kazi ya kuhesabu watu haitaathiri shughuli za uchumi au jamii kwani makarani wa sensa watapita katika kila kaya na kila mtu atakaelala nchini usiku wa sensa atahesabiwa mara moja na si zaidi ya hapo.”alisema
Aidha Aliwataka wakufunzi hao kuwa makini watakapokuwa wanakusanya taarifa hizo kwa usahihi kadri ya Maelekezo ya Dodoso fupi na refu Alisema uingizwaji wa takwimu za sensa kwenye komputa utafanikiwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa kama iliyotumika katika sensa ya mwaka 2002, teknolojia ambayo ilipata mafanikio makubwa ya kutoa matokeo ya
awali ndani ya miezi mitatu mara baada ya kuhesabiwa watu.
Wilaya ya Masasi ni wilaya moja ya Mkoa wa Mtwara Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 442,573.

About Author

Advertisement

 
Top