Unknown Unknown Author
Title: Liverpool yaizawadia Man.City, Huku L.Messi akifunga Bao La NNe La Liga
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kosa la beki Martin Skrtel lilimzawadia Tevez na Man.City pointi moja ugenini na fursa ambayo hawakustahili kuondoka na hata alama uwanja wa...
Kosa la beki Martin Skrtel lilimzawadia Tevez na Man.City pointi moja ugenini na fursa ambayo hawakustahili kuondoka na hata alama uwanja wa Anfield.
Liverpool ilionekana kama itakayompa furaha kocha wake mpya Brendan Rodgers kwa ushindi wa kwanza wa msimu hadi beki huyo Skrtel alipoamua kiuzembe kuurudisha mpira kwa golikipa bila kumuona Carlos Tevez, aliyekua akitegea na akaipokea zawadi hio bila kusita zikisalia dakika 10 za mchezo kumalizika. Hilo likawa bao lake la 100 katika Ligi ya England.
Kabla ya kosa hilo beki huyo Skirtel aliipatia Liverpool bao lake la kuiinua kabla ya kosa hilo na mchanganyiko wa mabeki uliomwezesha Yaya Toure kusawazisha.
Mkwaju wa ''free kick'' kutoka guu la Luis Suarez liliwarejeshea mashabiki wa Liverpool matumaini kabla ya kosa la Skrtel kuikoa City na kumnyongonyeza kocha Rodgers aliyeganda katika kiti chake.

Katika mechi nyingine ya siku Stoke ilishindwa kutumia uwanja wake wa nyumbani kuichapa Arsenal na mechi kumalizika kwa suluhu. Hivyo Arsenal ikacheza mechi yake ya pili bila kutikisa nyavu za adui il hali Stoke nayo ikicheza mechi ya pili kwa kumaliza kwa suluhu.
Lionel Messi scored a pair of late goals Sunday as Barcelona came from behind to win 2-1 at Osasuna in the Spanish league.
Barcelona's loss at Osasuna's Reyno de Navarra Stadium last season played a part in the Catalan club losing the title to Real Madrid, and the hosts looked destined for another win after Joseba Llorente's acrobatic 17th-minute goal.
Katika La Liga huko Uhispania mshambuliaji wa klabu ya Osasuna Juan Francisco Martinez alipiga mpira uliogonga besera huku kocha wa Barcelona Tito Vilanova akiamrishwa kuondoka uwanjani lakini Messi alipopokea pasi kutoka kwa Alexis Sanchez alifunga bao la kusawazisha mnamo dakika ya 76.
Klabu ya Osasuna ilibaki na wachezaji 10 baada ya Francisco Punal kuonyeshwa kadi nyekundu kwa ubishi wake na refa kuwa Messi alikua kaotea.
Baadaye Messi akapokea mpira kutoka kwa Jordi Alba katika dakika ya 80 na kuipatia klabu yake ushindi na bao lake la nne la msimu.








About Author

Advertisement

 
Top