THEO WALCOTT AANZISHA MGOMO KAMA WA RVP-ARSENAL

Theo WalcottTHEO WALCOTT bado hajasaini mkataba mpya Arsenal. Na kuna wasiwasi kwamba winga huyo wa kimataifa wa England atakuwa mchezaji mwingine mwenye jina kubwa kuondoka Emirates baada ya Robin van Persie kutimkia Manchester United.

Kocha wa Arsenal, Wenger amesema: “Bado tunajaribu kuuongeza mkataba wake.”

Wenger amempoteza Manahodha wake, Van Persie na Cesc Fabregas katika miezi 12 iliyopita, wakati kiungo Alex Song yupo karibu kuhamia Barcelona kwa ada ya pauni Milioni 15.

Walcott, aliyezaliwa miaka 23 iliyopita, amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake na Wenger amesema: “Wakati mchezaji hataki kubaki, unamlazimisha au unamuacha aondoke.”

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post