SINTA NA OKWI KUSHNEI!!!

sinta and joket Sintah na  Okwi  wamekuwa wapenzi  wa muda mrefu japo penzi lao  wamelifanya kuwa la siri......

Ugomvi kati yao umeibuka baada ya Sintah  kumkana OKWI  pindi alipoulizwa   na kituo  kimoja  cha  TV  jana Ijumaa   kama  anapenzi au  hana....

Pamoja  na kuulizwa   kwa zaidi  ya  mara  tatu,  Sintah alikataa  kuwa  hana  mpenzi.

Kitendo hicho kilimkera  EMANUEL  OKWI na ndipo  alipoamua kmpigia Simu   Sintah  akimuuliza  sababu   za  kumkana  hadharani.

Habari zinadai kuwa ,Okwi aliamua kukata simu, na tangu  jana  hadi  leo  hataki tena  kuwasiliana na Sintah.

Madai  haya ya ugomvi  yamethibitishwa na  Sintah mwenyewe  leo  baada   ya kuandika katika mtandao wake akielezea  jinsi alivyoumbuka.

"....Sasa pale nilipomkana mtu fidenge mama weee nilikuta missed call 20 .Haaaa yaani wewe utanikanaje kwenye kadamnasi vile

Uwiiiiii,,sasa nina anza moja kubembeleza. Yaani mwanaume ni kama mtoto mmh,naanza unajua sio hivyo naona aibu kwenye kioo

Leo nimekula mnuno mwanzo mwisho maana kila asubuhi nimezoea kuamshwa na kubembelezwa  ila leo kushnehi mpaka dakika hii si simba wala yanga bila bila,".....ALIANDIKA SINTAH

source: sintah.com

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post