Unknown Unknown Author
Title: AKAMATWA NA MABOMU NYUMBANI KWAKE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Jeshi la polisi mkoani Tabora, linamshikilia mkazi wa kijiji cha Ilolangulu kwa tuhuma za kukutwa na mabomu manne ambayo alikuwa ameyachimbi...
Jeshi la polisi mkoani Tabora, linamshikilia mkazi wa kijiji cha Ilolangulu kwa tuhuma za kukutwa na mabomu manne ambayo alikuwa ameyachimbia chini nje ya nyumba yake.
kamanda wa Polisi mkoani Tabora, ACP Antony Rutta, amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Nsimbi Masaki (30) ambaye alikamatwa kutokana na taarifa zilizotolewa na msiri wa Polisi ambaye alimuona akiwa na mabomu hayo.
Alisema mtuhumiwa huyo alipokamatwa alitoa ushirikiano  na kuonyesha sehemu aliyokuwa amyahifadhi mabomu hayo na ambayo alisema yalikuwa yamehifadhiwa kitaalam na yasingeweza kuhatarisha maisha katika eneo husika.
Alisema mtuhumiwa huyo aliyekuwa ameyachimbia chini mabomu hayo na kuyafunga kwa mifuko ya rambo na Plastiki anaoonekana ni mtaalam wa kuhifadhi mabomu na kwamba ni mtu mwenye uzoefu kwani kama asingekuwa na utaalam yangeweza kumlipukia.
Alisema kwa mujibu wa vyanzo vya polisi mabomu hayo yalikuwa yatumike katika matukio ya uhalifu na kwamba polisi wanaendelea kufanya mahojiano zaidi ili kujua mabomu hayo yalipokuwa yametokea ama njia yaliyopita kuingia nchini kwani yanadaiwa kutoka nchi jirani.
Katika tukio lingine Jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja kutokana na tuhuma za kukutwa na bunduki aina ya Gobore lakini ikiwa na uwezo wa kutumia kwa ufasaha risasi za shortgun na hivyo kuhisiwa kuwa inatumika katika matukio ya uhalifu.

kamanda Rutta, hata hivyo hakuweza kutaja jina la mtuhumiwa huyo, lakini alisema pamoja na bunduki alikutwa na risasi za shortgun sita ambazo hazijatumika na maganda matatu ya risasi hizo ambayo yalikuwa yametumika.
Aidha alisema jeshi hilo linawashikilia watu wanane kwa tuhuma za kukutwa na lita 75 za pombe haramu ya gongo na mitambo mitano ya kutengeneza pombe hiyo katika eneo la ng'ambo mjini hapa.
Alisema watu hao wanatarajia kufikishwa mahakamani kwa kujibu tuhuma zinazowakabili mara baada ya upelelezi wa polisi kukailika.







About Author

Advertisement

 
Top