Leo tupo katika dimba la OLYMPIC mjini Kiev Ukraine kushuhudia timbwili la fainali ya EURO2012 kati ya Spain na Italy,mechi inatarajiwa kuanza ifikapo saa 2:45 kwa muda wa kule Kiev hiyo itakuwa saa 3:45 kwa mida ya hapa nyumbani Tanzania.KARIBUNI SANA WADAU TUJUMUIKE!!!
HISTORIA
Nchi ya kwanza kunyakua kombe la Euro ilikuwa ni URUSI wakati huo ikiitwa Muungno wa Kisovieti.Katika mechi ya fainali ya kwanza ya mashindano haya ,URUSI ilikutana na YUGOSLAVIA,Julai 10 mwaka 1960 katika uwanja wa Parc des Prince jijini Paris.Urusi waliipiga Yugoslavia bao 2-1 na kuondoka na kombe.
Waanzilishi wa mashindano haya Ufaransa imeshakuwa mwenyeji mara 2..1960 na1984. Mashindano haya ya EURO yalianza mwaka 1960 mwaka ambao shirikisho la vyama vya soka barani ulaya lilianzishwa rasmi..Michuano hii hufanyika kilia baada ya miaka 4 na hushirikisha nchi 52 wanachama wa UEFA ambazo baada ya mchujo hubaki nchi 16 ambzo hukutana kwenye fainali kama hizi zilizofanyika POLAND na UKRAINE mwaka huu.
SPAIN waliandaa fainali za Euro mwaka 1964,mwaka ambao walichukua kombe kwa mara ya kwanza.Kwenye mechi ya fainali SPAIN walikutana naURUSI kwenye uwanja wa SANTIAGO BERNABEU mbele ya watazamaji waliokadiriwa kuwa 100 000,huku Dikteta wa Wahispania Franco akiwa jukwani kushuhudia kipute.
ITALY wao walifanikiwa kuwa wenyeji wa fainali za Euro mwaka 1968,na wao,kama walivyofanya SPAIN walifanikiwa kulibakisha kombe nyumbani baada ya kuwapiga YUGOSLAVIA kwa jumla ya bao 3-1.Lakini mechi ya fainali ililazimika kuchezwa mara mbili baada ya ile ya kwanza kwisha kwa matokeo ya 1-1 na siku 2 baadae ilirudiwa ambapo kocjha wa ITALY alibadilisha mfumo na mbinu ambazo zilizaa ushindi wa bao 2-0
Kwa hiyo leo Spain wakibeba kombe watakuwa wamelibeba mara 3 katika ushiriki wao wa michuano hii na mara ya 2 mfululizo baada ya vijana wa Luis Aragones kulinyakua katika mashindano yaliyopita dhidi ya Germany kule Vienna, kwa bao pekee lilofungwa na Fernando Torres
Refarii wa leo ni Mreno Pedro Proenca ambae ametangazwa kuchezesha mechi ya leo siku mbili zilizopita.Baada ya kuchezesha mechi ya fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE kati ya BAYERN MUNICH na CHELSEA vyema UEFA wameona ni vyema wampe refa huyo mwenye umri wa miaka 41 nafasi tena aoneshe uwezo wake…tofauti na wengi walivyotegemea kuwa Muingereza Howard Webb ndie angesimama kati.
BARCELONA na JUVENTUS ndio vilabu vyenye wachezaji wengi kwenye fainali ya leo.huku BARCA wakiwakilishwa na. Valdés, Piqué, Busquets, Xavi, Iniesta, Cesc na Pedro..
JUVE wao wana, Buffon, Chiellini, Barzagli, Bonucci, Marchisio, Giacherini na Pirlo..kama BARCA watamaliza suala la JORDI ALBA mapema leo basi itakuwa ina wachezaji 8.
CHANZO: SAIDI NUHU facebook user