NIJUZE NIJUZE Author
Title: Fainali Urafiki Cup Dar kesho
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
BAADA ya vuta ni kuvute hatimaye chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kimekubali fainali ya Kombe la Urafiki kati ya Simba na Azam kufanyika kwenye...

BAADA ya vuta ni kuvute hatimaye chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kimekubali fainali ya Kombe la Urafiki kati ya Simba na Azam kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kesho saa 10:00 jioni.
Kiongozi wa Kamati ya Mashindano hayo chini ya Rais wa ZFA, Amani Ibrahim Makungu alisema baada ya majadiliano marefu wamekubaliana mechi hiyo kati ya Simba na Azam kuchezwa Dar es Salaam.
Makungu alisema wao wamekubali kwa moyo mmoja sasa mechi hiyo ifanyike Dar es Salaam Alhamisi kuanzia saa 10 jioni na waamuzi pamoja na mgeni rasmi wa pambano hilo wote watatoka Zanzibar.
"Mechi haijauzwa ila ZFA wamekubali kuhamisha mechi hii kutokana na Simba na Azam zote kugoma kucheza uwanja wa Amaan," alisema Makungu.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu alisema tangu awali walikataa kushiriki mashindano hayo kwa sababu ya ubovu wa uwanja wa Amaan, lakini waandaaji wakaliwahakikishia kwamba suala hilo litashughulikiwa.
“Hatuwezi kuendelea kucheza mpira kwenye Uwanja huu kwa sababu ni mbovu, haufai kabisa unasababisha majeraha kwa wachezaji wetu, hasa ukizingatia kwamba mbele yetu tunakabiriwa na mashindano ya Kombe la Kagame,”alisema Kaburu.
Kaburu aliungwa mkono na Meneja wa Azam, Patrick Kahemele ambaye alisema wachezaji wao wamekuwa wanapata majeraha kila wanapocheza mechi kwenye Uwanja wa Amaan.
Wakati huohuo; Kocha mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic amesema tayari amepata kikosi cha kwanza atakachokitumia kwenye fainali ya Kombe la Ufariki dhidi ya Azam pamoja na Kombe la Kagame.
Tangu kuanza kwa mashindano ya Urafiki visiwani Zanzibar kocha Milovan amekuwa kwenye harakati za kujaribu wachezaji wake wapya kwa kuwapanga katika nafasi tofauti ili kutengeneza kikosi bora cha kwanza.
Akizungumza na Mwananchi, Milovan alisema ametumia mashindano ya Urafiki yanayofikia kikomo kesho kwenye Uwanja wa Amaan kupata kikosi hicho.
"Tayari ninacho kikosi cha kwanza kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Kagame na mashindano mingine yanayotukabili,"alisema Milovan.
"Kupitia mashindano haya nimefanikiwa kupata kikosi bora cha kwanza mbali na hivyo ninao wachezaji wasiopungua 15 walio tayari, kuziba mapengo yote yatakayojitokeza," alisema Milovan.
Milovan aliwataja, Haruna Moshi 'Boban', Felix Sunzu, Mwinyi Kazimoto na Juma Nyosso aliowatumia msimu uliopita kuwa bado wana nafasi kwenye kikosi hicho.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top