Kwa muda mrefu kumejengeka tabia ya waandishi ya habari za michezo kutoa uchambuzi wa michezo kwa kutegemea matokeo ya mechi husika.Mathalani ikitokea siku timu imeshinda, mchambuzi atatoa uchambuzi wenye kuonyesha ubora au uimara wa timu iliyoshinda huku mapungufu yakiwekwa kapuni (hata kama mapungufu yalikuwepo mengi tu). Wachezaji watapambwa na kusifiwa pasipo kifani utafikili walicheza mpira kama ule tunaoushuhudia ukichezwa na timu bora barani ulaya! Vilevile, wachambuzi hawa wamekuwa na mtazamo wa kuangalia performance ya mchezaji mmoja mmoja zaidi, wakati mpira wa kisasa unategemea zaidi timu kucheza pamoja yaani teamwork. Kuna timu zina wachezaji hawana majina makubwa lakini zinaogopwa kwa mchezo wao wa pamoja. Mfano mmoja ni Napoli ya italia! Kwa bongo si ajabu kusikia timu haikushinda kwa sababu mchezaji fulani alikosekana!
Lately kumekuwa na habari kwenye media eti national team jana haikushinda kwa sababu mbwana samatta hakuwepo. Napingana na hoja hii. Hiyo ni short sight, huyo ni mtu mmoja na sio kweli kama ana uwezo kama inavyoelezwa. Waandishi na wachambuzi hawa wanapaswa kuwa makini na wanayoyaongea. Wakati wa maximo wananchi wakisukumwa na waandishi/wachambuzi hawahawa walikuwa wakimshinikiza kocha kuchagua wachezaji fulanifulani. Leo hii watu haohao wanamponda mzungu pulsen wanasema afadhali ya maximo!. Jamani huyo mzungu habahatishi! hiyo ni taaluma yake kaisomea! Huyo ni mtaalam wa ngazi ya juu haitaji wiki nzima kumtazama mchezaji na kujua kama anamfaa au la!. Kwa mtazamo wangu, mwalimu alipata fursa ya kumwona samatta na naamini hata maamuzi ya kumwacha yalizingatia uchambuzi wake wa kitaalam kama mwalimu. Siamini kama angeweza kumwacha tu pasipo na sababu ya msingi, kwani timu ikishinda ni sifa kwake pia!.
Kwa upande mmoja tunatambua kuwa waandishi/wachambuzi wanapaswa kuandika au kusema! Kwao hii ni kazi! Na naamini wanalipwa kwa kazi hiyo! Hivyo ni lazima waseme au waandike! Lakini kwa upande wa pili naamini waandishi wana jukumu la kutoa taarifa sahihi pasipo kupotosha umma. Na ili waweze kutoa taarifa sahihi wanapashwa wajielimishe ili wajenge 'competence' kwenye eneo hili. Kwani si kila mtu anaweza kuandika habari za michezo, ni lazima awe amepata taaluma ya michezo! Jamani michezo ni taaluma inasomewa kama zilivyo taaluma zingine. Nimesema hivi kwa sababu ni rahisi kwa mwananchi wa kawaida kuamini kile anachokisoma au kukisikia kwenye media.
Mtazamo wangu kuhusu michezo hapa nchini ni kuwa tunahitaji kufanya uchambuzi mpana zaidi wa mfumo mzima wa mpira nchini na kuufanyia kazi. Mfano Je kuna Sera na Mkakati na Programu kuhusu michezo? Je kuna mfumo wa kitaasisi wa kutekeleza sera, mkakati na program? Je mfumo unakidhi au unahitaji maboresho? Je sera, mkakati na program vinatafsiriwa vipi kivitendo? Je mfumo unatoa fursa ya utambuzi, ukuzaji na uendelezaji wa vipaji? Muundo wa timu zetu ukoje? Je mfumo wa timu zetu unatoa fursa ya utambuzi, ukuzaji na uendelezaji wa vipaji?
Vinginevyo hizi hadithi za kulaumu makocha na wachezaji hazitaisha NG'O!
Mdau wa Michezo,
George
SOURCE: SHAFFIHDAUDA.COM