Mchezaji wa zamu Sergio Aguero alipata bao dakika za mwishomwisho na kuiwezesha Manchester City, baada ya kufungwa, hatimaye kuweza kujikakamua na kupata ushindi wa magoli 2-1 ilipocheza na Porto ya Ureno, usiku wa Alhamisi, ikiwa ni mechi ya mkondo wa kwanza wa mechi ya ligi ya Europa, kati ya timu 32 ambazo bado zimo katika mashindano.
Porto, ikicheza katika uwanja wa nyumbani, ilikuwa imetangulia kwa kupata bao kupitia Silvestre Varela. Lakini wageni Man City walipata nafasi ya kusawazisha wakati Alvaro Pereira alijifunga mwenyewe kwa kuuelekeza mpira kwa bega hadi wavuni, kufuatia mkwaju kutoka Yaya Toure, mpira ambao alitazamia utamfikia Balotelli.
Tags
Europa Leage