CAF YATOA RATIBA YA LIGI YA MABINGWA NA SHIRIKISHO

image Shirikisho la soka barani Afrika - CAF limetoa ratiba michuano ya kombe la ligi ya mabingwa wa afrika pamoja na kombe la shirikisho.

Wawikilishi wa Tanzania katika kombe la klabu bingwa ya afrika Yanga wamepangwa kuanza na Zamalek ya Misri na mshindi kati yao atacheza dhidi ya Missile ya Gabon au African Sport ya Ivory Coast, huku Mafunzo ya Zanzibar wakianza dhidi ya Muculmano ya Msumbiji na endapo watashinda watakutana na Dynamo ya Zimbabwe.

Klabu ya Simba ya Tz ambayo ni wawikilishi wetu katika kombe la shirikisho wenyewe wamepangwa kuanza na Kiyovu na Rwanda na mshindi wa mechi kukutana na Estif ya Algeria, huku Jamhuri la Zanzibar wakianza na Hwange ya Zimbwabwe na mshindi wa mechi hii atacheza na Amal ya Sudan.

BOFYA HAPA KUPATA RATIBA MPYA

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post