NIJUZE NIJUZE Author
Title: ZITO AIONYA SERIKALI
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
ASEMA BILA MUAFAKA CHAMA CHAKE KITATAFUTA NJIA MBADALA. WAKATI mjadala wa Muswada wa Sheria ya Kuunda Katiba Mpya ukizidi kuitikisa Serikal...

ASEMA BILA MUAFAKA CHAMA CHAKE KITATAFUTA NJIA MBADALA.
WAKATI mjadala wa Muswada wa Sheria ya Kuunda Katiba Mpya ukizidi kuitikisa Serikali, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ameonya kwamba kama suala hilo litachezewa, chama chake kitatafuta njia mbadala kwa wananchi ya kupata Katiba. Mjadala kuhusu muswada huo unakabiliwa na upinzani mkali kutoka ndani na nje ya Bunge na jana wabunge wengi wa CCM waliochangia, waliwashambulia wenzao wa Chadema.
Wabunge hao wa CCM, juzi walifanya kikao cha chama hadi saa 6:00, pamoja na mambo mengine kujadili namna ya kupitisha muswada huo. Kamati Kuu ya Chadema nayo ikikutana kwa dharura kujadili suala hilo. Zitto ambaye amerejea siku tatu zilizopita akitokea India alikokuwa akipatiwa matibabu, alisema jana katika mahojiano maalumu na gazeti la mwananchi kwamba, njia mwafaka ya kutafuta suluhu ni kwa viongozi wa Serikali kukubali kukaa meza moja na Chadema.
Alionya kuwa endapo itaendelea na mchakato huo wa Katiba bila mwafaka, mchakato huo utakuwa umekosa uhalali wa kisiasa kitu ambacho alisema ni hatari kwa nchi. Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni alionya kuwa bila kufikiwa kwa hatua hiyo, jambo hilo litazua mtafaruku  kwa sababu Chadema nacho kitaandaa mchakato wake wa kuunda Katiba Mpya.
“Si lazima yote wanayoyataka Chadema yakubaliwe na wala siyo lazima yote wanayokataa upande wa Serikali ya CCM yakubaliwe. Ni lazima pande zote zikubaliane. Ni lazima ifahamike kwamba mchakato wa Katiba Mpya ni muhimu sana hivyo maridhiano ya namna ya kuipata ni jambo ambalo halipaswi kupuuzwa.”Zitto alisema tukio la wabunge wa Chadema na NCCR Mageuzi kususia muswada huo bungeni, linaonyesha kuwa wabunge wa vyama hivyo vya upinzani hawako tena tayari kushiriki kwenye mchakato huo ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiupigania hasa baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu uliopita.
Alisema suala la kuunda Katiba Mpya ni la wananchi na wala siyo la kisiasa kama linavyopotoshwa na baadhi ya wanasiasa nchini.Kuhusu malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na baadhi ya wanasiasa hasa wa CCM kuwa Chadema kina ajenda ya siri ambayo inaweza kuipeleka nchi kwenye matatizo, Zitto alisema kinachoonekana kwenye mvutano huo ni kwamba makundi mbalimbali hayaaminiani kwenye mchakato huo.Alisema katika mchakato huo:
“CCM wao wanataka kujenga mazingira ambayo yatawapa nafasi ya kuendelea kuwapo madarakani na wakati huo upinzani nao unataka yawapo mabadiliko yatakayojenga uwiano ulio sawa na unaoweza kuwapa nafasi ya kuingia madarakani.”Katika mazingira ya namna hiyo, Zitto alisema linaweza likaundwa baraza la kitaifa ambalo litashirikisha wajumbe kutoka makundi mbalimbali, hasa Serikali na viongozi wa vyama.
Alisema kamwe suala hilo haliwezi kupata mwafaka kwa kuangalia wingi wa wabunge bungeni kwa sababu hali hiyo itachukua mkono wa itikadi za kisiasa.Zitto alisema kwa mazingira ya sasa ambayo CCM ndicho chama tawala na chenye idadi kubwa ya wabunge ni rahisi suala la Katiba kutekwa kwa maslahi ya chama hicho na kusahau kuwa ni jambo linalomgusa kila Mtanzania.
Alisema mabadiliko ya Katiba ni muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho viongozi wengi wa Serikali wamekuwa hawatekelezi wajibu wao ipasavyo na inakuwa vigumu kuwaondoa kwenye nafasi zao.Zitto alitoa mfano kuwa katika hatua za mwanzo za Kenya kutumia katiba yao mpya, imezuia uteuzi holela wa viongozi kushika nyadhifa nzito kama vile jaji mkuu na kuwaondoa baadhi ya viongozi  ambao wanatuhumiwa kwa rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top