NIJUZE NIJUZE Author
Title: MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI LINDI.
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mbio za mwenge zikiendelea mkoani hapa, Leo mwenge huo wa uhuru unaingia Manispaa ya Lindi ukitokea Wilaya ya lindi vijijini na Kakabidhiwa ...

DSC01113Mbio za mwenge zikiendelea mkoani hapa, Leo mwenge huo wa uhuru unaingia Manispaa ya Lindi ukitokea Wilaya ya lindi vijijini na Kakabidhiwa kwa mh mkuu wa wilaya ya lindi ambae ndio aliyekabidhi pia kwa kuwa ni mkoa ina mkuu wa wilaya mmoja hivyo alijikabidhi katika sherehe hizo ambazo zilifanyika Viwanja vya Shule ya msingi Mnazi mmoja. Mwenge huo ulifungua Jengo la Ofisi ya Kata ya Mingoyo ambalo linaendelea na Ujenzi.DSC01114

Hoa ni baadhi ya Viongozi waliojitokeza kuulaki mwenge wa uhuru katika sherehe za Mapokezi katika Viwanja Vya shule ya Msingi Mnazi Mmoja. wakiwa waheshimiwa madiwani na watendaji wa mitaa wakiwa na sare zao kama ada.DSC01116

Itifaki ilizingatiwa hapo kiongozi wa mwenge akivalishwa skafu na Chipkizi mara baada ya makabidhiano baina ya Lindi vijijini na manispaa ya Lindi Kushoto kwake ni Mh. Mkuu wa Wilaya ya Lindi.

DSC01118

Pia Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge alipokea zawadi kwa niaba ya wakimbiza mwenge wa uhuru wote kutoka kwa Chipkizi Hao.

DSC01119

Gwaride lilianza la mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kama ilivyo ada mara baada ya makabidhiano kati ya Wilaya na Manispaa na walianza kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa na Kufuatia na maafisa wa serikali na Waheshimiwa Madiwani wote walio hudhuria sherehe hizo za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mnazi Mmoja. Mwenge huo utakuwepo siku ya leo na kukesha katika viwanja vya shule ya msingi mpilipili na  kuondoka hapo kesho asubuhi kuelekea airpot tayari kwa safari ya Visiwani.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top