NIJUZE NIJUZE Author
Title: Manchester City kileleni
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Manchester City imetumia mwanya wa Man United kuteleza kwa kwenda kileleni baada ya kuizaba Aston Villa 4-1. Kipa wa Man City, Joe Hart al...

image

Manchester City imetumia mwanya wa Man United kuteleza kwa kwenda kileleni baada ya kuizaba Aston Villa 4-1.

Kipa wa Man City, Joe Hart aliokoa mkwaju wa Gabriel Agbonlahor mapema, kabla ya Mario Balotelli kufunga goli maridadi la kwanza.

Adam Johnson aliandika bao la pili baada ya Stephen warnok kufanya makosa, huku Vincent Kompany akiandika bao la tatu baada ya kuunganisha mpira wa kona.

James Milner alifunga goli la nne la City, na goli la kufutia machozi la Aston Villa lilifungwa na Stephen Warnock.

Kwingineko Norwich City imepata ushindi baada ya kuichapa Swansea 3-1. Anthony Pilkington alifunga magoli mawili ya Norwich, jingine la tatu likifungwa na Russell Martin. Goli ya Swanze lilifungwa na Danny Graham.

QPR ilitoka sare ya 1-1 na Blackburn Rovers, Heidar Helguson akifunga bao la QPR na Chris Samba akiandika bao la kusawazisha.

Stoke City walipata ushindi mnono baada ya kuichapa Fulham 2-0. Jonathan walters na Rory Delap wakifunga mabao hayo.

Wigan nayo ikicheza nyumbani ilipata kichapo cha 3-1 na Bolton. Nigel Reo Coker, David Ngog na Chris Eagles wakifunga magoli ya Bolton, na bao la kufutia machozi la Wigan lilifungwa na Mohamed Diame.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top