NIJUZE NIJUZE Author
Title: Yanga, Kagera Sugar kumuezi Nyerere leo
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
WAKATI Tanzania ikiadhimisha kumbukumbu ya miaka 12 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo kutashudia mabingwa wat...

image

WAKATI Tanzania ikiadhimisha kumbukumbu ya miaka 12 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo kutashudia mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Yanga wakishuka dimbani kuwakaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo iliyokuwa ifanyanyike kesho, lakini Shirikisho la Soka Tanzania TFF kwa kushirikiana na klabu hizo mbili Yanga na Kagera Sugar walikubalia kurudisha nyuma siku moja ili kutoa nafasi kwa mashabiki wa soka kumuezi Nyerere kwa kutazama mchezo huo.

Yanga iliyokusanya pointi 12, katika michezo nane itawavaa Kagera Sugar bila nyota wake wawili, Devis Mwape na kipa Yaw Berko ambao ni majeruhi.

Pamoja na kuwa na majeruhi, Yanga bado ina nafasi ya kushinda mchezo huo kutokana na rekodi yake ya ushindi kila inapocheza na Kagera Sugar.

Kocha wa Yanga, Sam Timbe alisema kuwa mechi ya leo kwa upande wake itakuwa ngumu na uenda akawakosa wachezaji wake wawili ambao ni Mwape na Berko.

''Nina majeruhi wawili tu, lakini kwa upande wa Berko nitamuangalia kwenye mazoezi ya leo (jana) jioni kuona hali yake kama itaendelea vizuri na kesho kama ataamuka vizuri naweza kumtumia lakini mpaka sasa siwezi kusema kama nitamtumia,'' alisema Timbe.

Alisema nia yake ni kuakikisha anashinda mchezo huo na kuendeleza rekodi yake ya ushindi ili kusogea kileleni mwa ligi baada ya kufanyia kazi makosa madogo madogo.

Naye kocha msaidizi wa Kagera Sugar, Mrage Kabange alisema wao kwa upande wao wamekuwa wakifanya maandalizi ya kutosha kujiandaa na mchezo huo na hakuna majeruhi katika kikosi chake.

Kabange alisema wanataka kufanya maajabu na kuvunja mwiko huo kwa kuwafunga Yanga kwao.

''Ni kweli Yanga wamekuwa wakitusumbua sana tukikutana nao, lakini wanatakiwa kujua kuwa kila siku sio Ijumaa japo lolote linaweza kutokea,'' alisema Kabange.

Alisema vijana wake wamekuwa na shauku kubwa kuakikisha wanarudi Kagera na pointi tatu na hawataki kupoteza mchezo kwani wanajua ligi inavyokwenda ndio inazidi kuwa ngumu.

Kagera Sugar inashika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 11, wakiwa nyuma ya yanga kwa pointi moja katika ligi hiyo inayoongozwa na Simba yenye pointi 19 baada ya kucheza mechi tisa.

Kesho Azam inayoshika nafasi ya pili watakuwa wageni wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Chamazi mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na viwango vya timu hizo walivyokuwa navyo msimu huu.

Vinara wa ligi Simba wenyewe watashuka dimbani Jumapili kucheza African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top