LINDI BUS STAND


Leo napenda kuiangalia Stand yetu ya Manispaa ya Lindi ambayo inahudumia wilaya na vitongoji vyake, kitu ambacho kimenivutia leo kukuletea hili ni mpangilio wa stand hiyo kwa shughuli za usafirishaji wake kwani hakuna mchanganyika wa magari (maeneo yanakoelekea) kila line ina Ruti yake hilo nijambo ambalo limenivutia sana kwani inamwondolea adha msafiri kujua kama natakakwenda Mtwara nielekee wapi kama Ninaelekea Nyangao nielekee wapi hiyo safi sana Big Up Manispaa ya Lindi.

Huu ni wakati wa Asubuhi ambapo Mishemishe inakuwa mingi kwa ajili ya Usafiri wa Kwenda Dar katika Stand yetu ya Manispaa, lakini kitu kilicho nishtua ni kuona hawa akina mama wanaotoa huduma ya kifungua kinywa hapa katika eneo la stand kiukweli inasikitisha hawana sehemu ya au ndo wameamua kufanyia hapa biashara zao na je ni sahihi kufanya hivyo ukiangalia kiafya je bwana afya ameliona hili na je amechukua Hatua gani? Juzi nilisikia baadhi ya hoteli zilifungia kufanya shughuli zao za huduma kama hii kwa kuwa mazingira yao yalikuwa hayalidhishi je? haya yanaridhisha kwani Wanasiku nyigi hawa watu wakifanya shughuli zao

Katika eneo Hili. Mbaya zaidi ukiangalia kunauzio unaoonyesha Ujenzi unaendelea maana yake kutakuwa na vumbi na unakuta vyakula viko wazi je Hili ni sawa na kama hawana maeneo utaratibu ukoje.

Ukiwa nje ya geti la kuingia ndani ya stendi unakuta Bajaji, Boda Boda zikisubiri wateja hawa nawapongeza kwani unakuta wamekaa kwa mpangilio kama waonekanavyo kwenye picha Hapo Pembeni na Hapo chini

Pia eneo zima likiwa safi kabisa nawapongeza tena Halmashauri ya Manispaa kwa kuzingatia Usafi unafanyika katika stendi hiyo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post