AMCOS ZA PWANI ZATAKIWA KUACHA KUWA NA OFISI ZA KWENYE MABEGI.

Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika cha Pwani (CORECU), Mussa Hemedi mng'eresa akiteta jambo na viongozi wa AMCOS za Pwani wakati wa ziara ya Mafunzo katika AMCOS za wilaya ya Ruangwa, Nachingwea na Liwale.
 
Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika RUNALI Odas Mpunga akizungumza na viongozi wa AMCOS za mkoa wa Pwani namna gani uwepo wa ofisi na vitega uchumi vilisaidia kuleta maendeleo katika AMCOS za wilaya ya Ruangwa, Nachingwea na Liwale.
Viongozi na Wadau wa ushirika wakiwa Wilaya ya Liwale ziara ya Mafunzo katika AMCOS za wilaya ya Ruangwa, Nachingwea na Liwale. 

Na. Fredy Mgunda, Lindi

Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika cha Pwani (CORECU), Mussa Hemedi mng'eresa amevitaka vya yote vya msingi katika mkoa wa Pwani (CORECU) kuhakikisha vinajenga ofisi ili waweze kuwahudumia wakulima ipasavyo.

Akizungumza wakati wa ziara ya mafunzo katika AMCOS za wilaya ya Ruangwa Nachingwea na Liwale,mng'eresa alisema kuwa AMCOS zote zinaofisi na zinahifadhi nyaraka na kuwahudumia wakulima katika ofisi hizo hivyo sasa ni zamu ya AMCOS za mkoa wa Pwani kujenga ofisi.

mng'eresa alisema kuwa mapato wanayopata vyama vya msingi katika mkoa wa Pwani yanalingana kwa kiasi kikubwa na mapato ya AMCOS zilizo chini ya RUNALI hivyo kila AMCOS mkoa wa Pwani wanatakiwa kuiga mifano ya vyama vya msingi vya Ruangwa, Nachingwea na Liwale kimaendeleo.

Aidha mng'eresa aliwapongeza RUNALI kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa kununua vyombo vya usafirishaji,ujenzi wa viwanda vidogo vidogo na ujenzi wa Hoteli ya kisasa katika wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Nao baadhi ya viongozi wa AMCOS kutoka mkoa wa Pwani walisema kuwa wamejifunza mengi yenye faidi kwa vyama vyao hivyo wataenda kubadili mtanzamo na kuvifanya vyama viwe vya kibiashara.

Walisema kuwa AMCOS za wilaya ya Ruangwa, Nachingwea na Liwale limepiga hatua kimaendeleo tofauti na wao huku mapato yakiwa yanalinga na kile wanachopa hivyo kilichobaki ni uthubutu tu wa viongozi kuamua maamuzi magumu ya kimaendeleo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika RUNALI Odas Mpunga alisema kuwa kwa kipindi cha miaka saba sasa wamejithatiti katika nyanja za kiuchumi hasa kwenye ujenzi hoteli ya kisasa, Maghala, usafirishaji, viwanda vidogo vidogo na ujenzi wa ofisi za chama kikuu kila wilaya ili kutoa huduma nzuri kwa wakulima na viongozi wa AMCOS zote

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post