NIJUZE NIJUZE Author
Title: WAZAZI NA WALEZI WASIOWAPELEKA WATOTO SHULE KUSHITAKIWA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga akiongea na wananchi wa kijiji cha Mkwajuni Januari 18, 2024 Na Ahmad Mmow,  Lindi. Serikali wilayan...
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga akiongea na wananchi wa kijiji cha Mkwajuni Januari 18, 2024

Na Ahmad Mmow,  Lindi.

Serikali wilayani Lindi imesema itawatafuta, kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wazazi na walezi ambao watoto wao hawajaripoti shuleni.

Hayo yameelezwa na mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga  jana kwanyakati na maeneo tofauti katika vijiji vya Mkwajuni na Nangaru  wakati wa hafla ya kumkabidhi mkandarasi maeneo ya mradi wa ujenzi wa miundombinu ya maji.

Ndemanga alisema kuna watoto ambao wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari, hatahivyo hadi sasa hawajaripoti. Kwahiyo serikali itawatafuta, kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wazazi na walezi wa watoto hao.

Amesema ni jambo lisilokubalika kuona watoto hao mpaka sasa hawaripoti shuleni. Kwahiyo serikali haiwezi kuvumilia hali hiyo iendelee.

Amebainisha kwamba serikali haitaingia gharama ya kuwakusanya na kuwasafirisha wazazi na walezi hao kwenda mahakamani. Badala yake mahakama itakwenda huko huko waliko. Ili baada ya kuhukumiwa wasafirishwe na kufikishwa magerezani moja kwa moja.

"Hatutaki kupata hasara ya kuwasafirisha kwenda mahakamani. Mahakama itahamia hukuhuku vijijini. Maana kwasasa mahakama zinatembea. Kwahiyo tutamalizana hukuhuku," alisisitiza Ndemanga.

Mkuu huyo wa wilaya ya Lindi aliwaasa wazazi na walezi hao ambao watoto wao hawajaripoti shuleni wahakikishe wanaripoti haraka kabla ya kukumbwa na zoezi la kuwakamata kuanza.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top