Na Ahmad Mmow, Lindi.
Waandishi wa habari wa mikoa ya Lindi na Mtwara wameaswa waepuke kupotosha habari.
Wito huo kwa waandishi hao umetolewa leo mjini Mtwara, na mkuu wa mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abass Ahmed wakati anafungua semina ya siku mbili kwa waandishi wa habari kuhusu uwasilishaji, usambazaji na uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Kanali Ahmed alisema waandishi wa habari hawanabudi kuandika taarifa sahihi na zenye ukweli badala ya kupotosha. Kwani jamii inahitaji kupata taarifa sahihi na zakweli.
Mkuu huyo wa mkoa wa Mtwara amesema wanahabari wanatakiwa waheshimishe tasnia ya habari kwa kuandika kwa usahihi na ukweli taarifa za matukio na mambo mbalimbali.
Aidha mkuu wa mkoa Ahmed aliwaasa wanahabari hao waepuke kutumika kwa masilahi binafsi ili kuwapamba baadhi ya watu ambao wanatamani kuandikwa vizuri kwa kupongezwa na kusifiwa tu.
"Baadhi ya watu wanachukia iwapo waandishi wa habari wataandika habari ambazo haziwapendezi. Hata kama habari hizo zinaukweli," alisisitiza Ahmed.
Ahmed ambae alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo, pia alitoa wito kwa waandishi hao waandike mambo yenye faida kwa jamii. Ambapo pia habari wanazoandika zijibu maswali ya kero zilizopo kwa jamii badala ya kuibua na kuacha maswali.
Aliweka wazi kwamba baadhi ya waandishi wanaacha kuandika habari zenye faida kwa jamii. Badala yake wanaandika habari zisizo na tija.Ikiwamo kuwapamba baadhi ya watu kwa masilahi binafsi.
Kwaupende wake Kamisaa wa sensa na makazi, spika msitahafu wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda aliwaasa waandishi hao watumie semina hiyo kujifunza kwa makini mambo yanayohusu takwimu ili waandike kwa weledi habari zinazohusu takwimu.
Alisema ni vigumu kuandika habari kwa waledi bila kujua kwa undani habari wanazoandika. Huku akiwahimiza wasome. Kwani uelewa utawafanya waandike habari sahihi na kweli.
Aliwatoa hofu waandishi hao wasiogope kuomba taarifa kwani zipo. Nakwamba taasisi ya takwimu inatambua umuhimu wa waandishi kuzijua takwimu.
WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUEPUKA UPOTOSHAJI
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abass Ahmed akizungumza na Wanahabari wa
mikoa ya Lindi na Mtwara wakati wa Ufunguzi wa Semina kuhusu
Uwasilishaji, Usambazaji wa matumizi ya matokeo a Sensa ya watu na
makazi waka 2022.
Kamisaa wa sensa na makazi, spika mstahafu wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akizungumza na Wanahabari wa
mikoa ya Lindi na Mtwara wakati wa Ufunguzi wa Semina kuhusu
Uwasilishaji, Usambazaji wa matumizi ya matokeo a Sensa ya watu na
makazi waka 2022
Wanahabari wa
mikoa ya Lindi na Mtwara wakifuatilia Ufunguzi wa Semina kuhusu
Uwasilishaji, Usambazaji wa matumizi ya matokeo a Sensa ya watu na
makazi waka 2022.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.