Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndg. Shaibu Ndemanga |
Na Ahmad Mmow, Lindi.
Mamlaka ya mapato nchini (TRA) mkoa wa Lindi imepongezwa kwa kukusanya kodi na kuvuka lengo bila kutumia nguvu.
Pongezi hizo zimetolewa leo mjini Lindi, na mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga wakati wa kilele cha wiki ya mlipa kodi.
Ndemanga ambae katika maadhimisho hayo alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Lindi alisema licha ya TRA mkoani humu kuvuka makadirio ya makusanyo ambayo yalikuwa shilingi bilioni 9.2 na kuvuka kiwango hicho kwa kufikia shilingi bilioni 9.6, lakini imeweza kukusanya bila kutumia nguvu na vitisho kwa walipa kodi.
Alisema miaka ya nyuma kulikuwa na migogoro mingi baina ya mamlaka hiyo na walipa kodi ambao wengi wao ni wafanyabiashara. Hatahivyo hivi sasa hali hiyo haipo.
Mkuu huyo wa wilaya ya Lindi alibainisha kwamba mafanikio hayo kwakiasi kikubwa yamechangiwa na kazi kubwa ya kutoa elimu kwa walipa kodi, ambayo imefanywa na watumishi wa mamlaka hiyo.
Afafanua na kuweka wazi kwamba kazi ya kutoa elimu imesababisha watambue umuhimu wa kulipa kodi bila shuruti. Huku wakitambua kwamba kulipa kodi ni wajibu wao wa msingi. Huku akitoa wito kwa mamlaka hiyo kutoa ushirikiano na walipa kodi.
"Miaka ya nyuma vikao vingi vilikuwa vya kutatua na kusuluhisha migogoro. Lakini sasa vikao nivya kujadiliana na kushauriana," alisema Ndemanga.
Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya by Lindi alitoa wito kwa mamlaka hiyo ijipange na kujiandaa kutumia fursa zinazotarajiwa kujitokea katika mkoa huu wa Lindi kipindi kifupi kijacho.
Aliitaja baadhi ya miradi inayotarajiwa kutoa fursa hizo kuwa ni ujenzi wa ndaki (kampasi) ya Dar-es-Salaam na ujenzi wa ndaki ya chuo cha usafirishaji(NIT).
"Msije mkaona kama mmevamiwa na fursa. Jiandaeni na jipangeni sasa, mkitumia fursa hizo mnaweza kuufanya mkoa wa Lindi kuwa miongoni mwa mikoa inayokusanya mapato makubwa na kuchangia pato kubwa kwa taifa," alitahadharisha na kusisitiza Ndemanga.
Kwa upande wake naibu kamishna wa uchunguzi wa TRA, Feliciana Nkane alisema mamlaka hiyo inawathamini walipa kodi, na sasa inaboresha mifumo na kuendelea kutoa elimu kwa walipa kodi ili wawe na uelewa wa kutosha kuhusu kodi.
Naibu kamishna huyo ambae alimwakilisha kamishna mkuu wa TRA alitoa wito kwa walipa kodi walipe kodi kwa wakati na wazingatie taratibu na sheria. Ikiwamo kuwasilisha taarifa kwa wakati, kutumia mashine za kiilektroniki (EFD) na kulipa kodi bila shuruti. Lakini alitoa wito kwa wananchi kudai risti wanapofanya manunuzi.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.