NIJUZE NIJUZE Author
Title: ROBERTINHO KWENYE PRESHA KUBWA SIMBA SC
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Licha ya kufanikiwa kuivusha Simba hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira y...

Licha ya kufanikiwa kuivusha Simba hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira yuko katika presha kubwa

Baada ya mchezo dhidi ya Power Dynamos uliopigwa uwanja wa Azam Complex jana na Simba kulazimishwa sare ya bao 1-1 matokeo ambayo yalitosha kuwapeleka Wekundu wa Msimbazi makundi kwa faida ya bao la ugenini, Bodi ya Wakurugenzi ya Simba ilikutana kwa dharura kujadili kile kilichoelezwa kutoridhishwa na kiwango cha timu

Msimu huu mashabiki wa Simba wametoa malalamiko karibu kila baada ya mechi kutoridhishwa na kiwango cha timu yao licha ya kupata matokeo mazuri

Hofu iliyopo ni kwamba hakuna uhakika kama Simba itaweza kufikia malengo yake ya kushinda nataji yote ya ndani pamoja na kucheza nusu fainali ya ligi ya mabingwa kama timu itaendelea kucheza kama ilivyo sasa

Miongoni mwa waliotoa malalamiko ni Rais wa heshima wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji ambaye kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii aliandika ujumbe unaoashiria haridhishwi na kile alichokishuhudia

Katika misimu iliyopita, Simba ilidumisha utamaduni wake wa kucheza kandanda safi iliyoambatana na ushindi na zaidi kwenye michuano ya Kimataifa Simba imejijengea heshima ya kuwa timu hatari sana inapocheza mbele na mashabiki wake

Robertinho amekuja na falsafa tofauti ambapo jambo muhimu kwake ni timu kupata matokeo mazuri pasipo kujali wamecheza vipi. Mpaka sasa Robertinho amefanikiwa katika mbinu zake, hajapoteza mchezo katika mechi tisa zilizopita

Mwanzoni mwa msimu huu aliiongoza Simba kutwaa Ngao ya Jamii na ameweza kushinda mechi zote tatu katika ligi kuu pamoja na kuipeleka Simba hatua ya makundi CAF CL

Hata hivyo presha ya mashabiki ambao hawaridhishwi na vile timu yao inacheza, imepata nguvu zaidi baada ya kuanza kuungwa mkono na baadhi ya viongozi

Pengine Robertinho na benchi lake la ufundi wanapaswa kufanya kitu haraka kwa kuanzia mechi inayofuata kwenye ligi kuu dhidi ya Prisons itakayopigwa Alhamisi huko Mbeya

Baada ya mechi hiyo Simba inakabiliwa na mechi mbili za AFL dhidi ya Al Ahly, mchezo wa kwanza ukipigwa Oktoba 22 uwanja wa Benjamin Mkapa na marudiano kupigwa Oktoba 24 huko Misri

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top