Dr. Gozbert Kamugisha ambaye ni Mwanzilishi Mwenza wa Taasisi ya Wanasayansi Chipukizi (Young Scientist Tanzania YST) akitoa hotuba wakati wa utoaji tuzo. |
Msomisi Mbenna Mshauri wa Masuala ya Kijamii kutoka Kampuni ya Shell Tanzania |
Wanafunzi washiriki katika tafiti mbalimbali kwenye picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Viongozi na mfadhili wa Mradi wa YST |
Na. Fungwa Kilozo, Lindi
Taasisi ya Wanasayansi Chipukizi Tanzania (YST) Young
Scientists Tanzania imekuwa Taasisi iliyojikita katika kuhamasisha na kukuza
maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini
kupitia mradi wa kuwajengea uwezo na ujuzi wanafunzi wa sekondari kwenye masomo
ya sayansi nchini.
Tangu mwaka 2013 kampuni ya Shell Tanzania wamefadhiri Mradi
huo wa kuwajengea uwezo na ujuzi wanafunzi wa Sekondari kwenye masomo ya
sayansi nchini unaotekelezwa na YST ili kuboresha sayansi katika shule za
sekondari.
Mradi huo Umewawezesha wanafunzi hao kuwa Wabunifu na
utamaduni wa kufanya tafiti ambazo zinakuwa na manufaa katika jamii zao na
Taifa kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa na Bi. Msomisi Mbenna ambaye ni Mshauri wa
masuala ya kijamii kutoka kampuni ya Shell Tanzania ambayo ni mfadhili wa mradi
huo wakati wa sherehe za utoaji wa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika
tafiti zao mwaka 2023 zilizofanyika Wama-Sharaf Manispaa ya Lindi, ambapo shule
mbili zitauwakilisha mkoa wa lindi katika Mashindano ya kitaifa Jijini Dar es
Salaam.
Shule 15 za Sekondari za mkoani wa Lindi zimeshiriki katika
kufanya tafiti mbalimbali. Shule zilizopata nafasi mbili za juu za kwenda
kuwakilisha mkoa kwenye mashindano ya Kitaifa yatakayofanyika Dar es Salaam ni
Kivinje Sekondari ya wilayani kilwa na Nkowe Sekondari ya Halmashauri ya
Ruangwa ambayo ndio ilikua namba moja.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.