Kuelekea kilele cha siku ya Ukimwi duniani, Kitaifa ikiadhimishwa katika mkoa wa Lindi Mamlaka ya Udhibiti na kupambana na Dawa za kulevya nchini DCEA kupitia ofisi ya Kanda ya Kusini inayojumisha mikoa ya lindi, Mtwara na Ruvuma wanashiriki maadhimisho hayo huku shabaha yao ikiwa ni kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara yatokanayo na dawa za kulevya.
Bi. Salome Mbonile, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Kanda ya Kusini Mamlaka ya Udhibiti na kupambana na Dawa za kulevya nchini DCEA |
Akizungumza na Lindiyetu Tv Kaimu Kamishna Msaidizi wa kanda ya kusini bi Salome Mbonile amesema kwa kiasi kikubwa dawa hizo za kulevya huingia nchini kwa kutumia ukanda wa bahari hivyo ukanda wa kusini upo kwenye hatari kubwa ya kupokea dawa hizo kutoka kwa nchi zalishaji.
"Kiasi kikubwa Dawa za kulevya zinaingia kupitia ukanda wa bahari hasa hasa wananchi tunawahitaji jufika hapa waweze kupata elimu ya dawa za kulevya, Takwimu zinaonesha mwaka 2021 tulikamata dawa za kulevya kiasi cha 859.39 ikujumuisha kilo 504.36 za Heroin na kilo 355 za Methamphetamine hiki ni kiasi kikubwa ambachokilikamatwa kwa mara moja hivyo kanda hii inahatari zaidi kuwa kwenye ukanda ambao dawa zinaweza kuingia kutoka kwa nchi zalishaji". Alisema Mbonile.
Bi Upendo Chenya Mfamasia Mamlaka ya Udhibiti na kupambana na Dawa za kulevya nchini DCEA |
Akizungumzia Matibabu kwa waathirika wa madawa ya kulevya bi Upendo Chenya amesema kupitia vituo vya Kinga Saidizi, Vituo vya Afya vya serikali pamoja na SOBER HOUSE wameweza kuwahudumia vyema kwa kuwapatia dawa mbadala ambazo zimeweza kuwasaida ambapo pia ameondoa ile dhana iliyopo kuhusu matumizi ya dawa ya methadone.
"Kwanza kabisa tatizo la uraibu ni tatizo kubwa na matibabu yake hutegemea na kiasi gani mgonjwa ameathirika, kwaiyo kuna matibabu mbalimbali moja wapo vipo vituo ambavyo vinatoa dawa ya methadone, Vituo vya Kinga Saidizi pamoja na Vituo vya Afya vya Serikali vyote vinaujuzi wa kuwasaidia wagonjwa walioathirika na dawa za kulevya.
"Dawa ya Methadone ni salama ambayo haimpi mgonjwa raha kwaiyo tunachokifanya ni kumtoa mgonjwa kwenye ugonjwa sugu ya dawa zisizo salama na kumpatia dawa salama ambayo inatolewa na wajuzi pia ikiwa kwenye kiwango stahiki na wanakuwa kwenye uangalizi wa karibu". amesema Bi Chenya.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.