Unknown Unknown Author
Title: WASAFIRISHAJI, WAINGIZAJI NA WAUZAJI WA DAWA ZAKULEVYA WAPEWA ONYO KALI NCHINI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa kitengo cha polisi cha kupambana na madawa ya kulevya nchini, kamishina msaidizi mwandamizi Mihayo Msihkela amewaonya wanaojihusis...
Mkuu wa kitengo cha polisi cha kupambana na madawa ya kulevya nchini, kamishina msaidizi mwandamizi Mihayo Msihkela amewaonya wanaojihusisha na vitendo vya uingizaji hapa nchini, uuzaji na usafirishaji wa madawa ya kulevya kwa kuwataka waachane na vitendo hivyo badala yake watafute shughuli nyingine za kuwapatia kipato halali kwa kuwa serikali imejipanga vizuri katika kukabiliana na watu hao.
Dawa za kulevya
Mkuu huyo ametoa onyo hilo baada ya kukutana na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama walioko kwenye mpaka wa Mtukula ulioko mkoani Kagera unaotenga nchi za Tanzania na Uganda ambao walipewa mafunzo maalumu na vitendea kazi vya kuthibiti uingizaji wa madawa ya kulevya kupitia katika mpaka huo, pia amehimiza maafisa wa idara za serikali walioko kwenye mpaka huo kufanya kazi kwa ushirikiano ili wadhibiti mianya yote ya uingizaji wa madawa ya kulevya hapa nchini.

Kwa upande wake, Christina Rweshabula ambaye ni mwanasheria wa tume ya kuratibu udhibiti wa dawa za kulevya amesema sheria zilizokuwepo ndizo zilikuwa zinachangia ongezeko la vitendo vya uingizaji wa madawa ya kulevya hapa nchini, naye Bundara Musiba mkuu wa kitengo cha intelijensia cha jeshi la polisi mkoani Kagera amesema mapambano dhidi ya madawa ya kulevya yatafanikiwa endapo wanaosimamia sheria watafanya kazi kwa kuzingatia maadili, huku Ulimbakisya Mwakalogo afisa uchunguzi wa tume ya kuratibu udhibiti madawa ya kulevya akieleza mbinu za kuyabaini madawa hayo.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top