TID, TUNDA NA WASANII WENGINE WATUHUMIWA WA MADAWA YA KULEVYA WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Takriban watuhumiwa 10 wa dawa za kulevya ambao ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu asubuhi ya Leo.
Watuhumiwa wa Madawa ya kulevya
Miongoni mwa waliofikishwa mahakamani ni wasanii Rommy Jones, TID, Babuu wa Kitaa, Petit Man, Tunda (model wa kike), Lulu Diva, Recho, Joan, na wengine.

Watuhumiwa wote wamesomewa kiapo cha Mahakama ambapo upande wa Jamuhuri umeomba watuhumiwa hao waamrishwe kuwekwa chini ya uangalizi kwa kuripoti polisi mara 2 kwa mwezi kwa kipindi cha miaka 2 ili kuangaliwa kama wameacha tabia ya kutumia dawa hizo hususani bangi.

Wakili wa upande wa utetezi amedai taarifa hizo hazijakamilika kwani hazioneshi wanaojiusisha na dawa za kulevya na walikamatwa lini na wapi na hakuna ushahidi wa kujitosheleza wa madai hayo kiasi cha wao kupata dhamana ya kuangaliwa tabia zao bila polisi kutoa ufafanuzi wa kina wa kwanini wanahitaji kupata dhamana ya uangalizi wa nidhamu.


UPDATE:
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa amri kwa TID na wenzake saba kufanya yafuatayo;

1. Kusaini dhamana (bond) ya Milioni 10.
2. Kuwa na tabia nzuri kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja.


Hivyo watuhumiwa wote wako huru wakishatia saini karatasi za Bond.

Bond

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post