Na. Ahmad Mmow, Kilwa.
Zana zilizokatazwa na sheria kutumika kuvulia zinazokisiwa kuwa na thamani ya takribani shilingi 12.00 milioni, jana ziliteketezwa kwa kuchomwa moto katika pwani ya Somanga wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kikundi cha ulinzi shirikishi wa rasilimali za bahari na pwani cha kata ya Somanga, Yusufu Mhani zana hizo zilizokamatwa hivi karibuni kupitia doria ya siku tatu kuanzia mwambao wa Somanga, Matapatapa hadi Mtoni katika bahari ya Hindi ni kokoro 16 nyavu za mishipi 6 dau moja ambalo limehifadhiwa.
Zana zote zikitajwa kuwa na thamani ya takribani shilingi 12,000,000. Akizungumza baada ya kuteketezwa zana hizo zilizokuwa zinatumika kwa uvuvi haramu, mkuu wa wilaya ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai alionya kwamba vita na mapambano yanayotokana na uvuvi haramu katika wilaya hiyo haitakwishwa hadi ushindi kamili upatikane.
Alisema kunakila sababu ya kuendeleza mapambano hayo ambayo msingi wake mkubwa ni kulinda maliasili na rasilimali zilizopo baharini kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Mkuu huyo wawilaya alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano katika kufanikisha azima ya serikali ya kukomesha vitendo hivyo vinavyotishia uwepo wa viumbe hai vilivyopo baharini na afya za walaji wa samaki waliovuliwa kwa kwa sumu, mabomu nk.
Alisema kunahaja na sababu za msingi za kuendeleza mapambano hayo. Akibainisha kuwa kumaliza samaki waliopo baharini ni sawa na kuzalisha watu wengine wasio na ajira wilayani humo. Kwasababu sekta ya uvuvi inatoa ajira kwa watu wengi.
"Mpaka sasa wavuvi wanaotambuliwa katika wilaya yetu ni 7200, wachuuzi ni 3500, kwahiyo hatuwezi kuacha ajira hizo zipotee kwa tamaa na uroho wa watu wachache wasio na huruma na binadamu wenzao na viumbe vingine," alisema kwa ukali.
Akitaja faida zilizopatikana tangu kuanza misako hiyo ni kuendelea kukamatwa zana za uvuvi haramu ambako kumepunguza kasi ya uvuvi huo, kuongezeka kwa kiwango cha upatikanaji wa samaki kwa wavuvi wadogo wadogo ambao vyombo vyao vya kusafiria havina uwezo wa kusafiri umbali mrefu na kuokoa usalama wa walaji wa samaki.
"Afya zenu wananchi wangu na za walaji wengine zitakuwa salama, ajira zitaongezeka, mapato ya halmashauri yetu yataongezeka pia. Lakini pia tutakuwa tumeokoa mazalia ya samaki kwahiyo tusaidiane, kuweni na uchungu na maliasili zenu badala ya kuwapokea na kushirikiana na wageni kuharibu".
Aidha Ngubiagai aliwataka wavuvi wasiosajiliwa na kukata leseni wahakikishe wanafanya mambo hayo ili kuepuka usumbufu ambao yeye asingependa utokee. Kwa madai kwamba nia ya serikali ni njema ya kuhakikisha kila mtu anapata mapato yake kwa kufanya kazi halali bila kuvunja sheria.
Huo ni muendelezo wa kukamatwa zana haramu za uvuvi katika wilaya hiyo, tangu mkuu huyo wawilaya atangaze operesheni ya kupambana na uvuvi haramu isiyokoma katika wilaya hiyo.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.