Unknown Unknown Author
Title: WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YENYE TIJA ,ILI KUPATA MAZAO YENYE BORA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro, wakati akifungua Maonyesho ya zana za kilimo katika viwanja vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo...
Maonyesho ya zana za kilimo
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro, wakati akifungua Maonyesho ya zana za kilimo katika viwanja vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani.
Maonyesho ya zana za kilimo
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Seliani Dr Daniel Mafuru   Akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo
Maonyesho ya zana za kilimo
Meneja masoko wa kampuni ya John Deere ambaye pia ndio wadhamini wakuu wa maonyesho haya Wayne Travas Akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari.
Maonyesho ya zana za kilimo
Afisa mauzo wa kampuni ya Irrico Saimoni Manyike akimuelewesha mkulima jinsi kampuni yao inavyofanya kazi ya kusambaza teknolojia ya umwagiliaji wa Matonye.
Maonyesho ya zana za kilimo
Katika maonyesho haya pia kamera yetu iliweza kumkuta mwimbaji mashuhuri wa jijini hapa Nakaya Sumari akiwa na Phidesia Mwakitalima nao pia walihudhuria katika maonyesho hayo ili nao waweze kulima kilimo chenye tija.
Maonyesho ya zana za kilimo
Washiriki ambao ni wakulima wakifuatilia kwa makini mada ambazo zilikuwa zikiendelea wakati wa ufunguzi.
Maonyesho ya zana za kilimo
Baaadhi ya wakulima wakiangalia matrekta ya kisasa yanayouzwa na kampuni ya John Deere nambao ni wathamini wakuu.
Maonyesho ya zana za kilimo
Afisa mauzo wa kampuni ya Irrico Saimoni Manyike akiwaonyesha wakulima hawapo pichani jinsi kilimo cha umwagiliaji wa mtone kinavyokuwa.

Na.Woinde Shizza, Arusha
Sekta ya kilimo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufugaji holela , ambao hupelekea uharibifu wa mazingira, Teknolojia duni pamoja na ugumu wa kupata mitaji ya kuboresha miundombinu ya kilimo.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro, wakati akiofungua Maonyesho ya zana za kilimo katika viwanja vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani vilivyopo ndani ya jijini Arusha ambapo ni mara ya kwanza kufanyika.


Alisema kuwa sekta ya kilimo inakabiliwa na changamoto za ufugaji holela ambao unasababishwa na wafugaji,wakulima kutumia teknolojia duni au zazamani katika ukulima pamoja na wakulima wengi kukosa mitaji ya kuboresha miundo mbinu ya kilimo.

Alisema kuwa hii inachangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha maendeleo ya sekta hii kutokana na wananchi wengi kutumia kilimo cha kawaida badala yakutumia kilimo cha kisasa ambacho kinaleta tija.
“hapa Tanzania zaidi ya asilimia 75% wanategemea kilimo lakini kati yao n asilimia 1.5 tu ndio wanatumia kilimo cha kisasa kama kilimo cha umwagiliaji, kupanda mbegu bora pamoja na kilimo cha matone hivyo ni vizuri wakulima wetu kujitaidi kutumia kilimo cha kisasa ili kuweza kufanya kilimo chenye tija ambacho kinamnufaisha yeye mkulima mwenyewe na kuachana na kilimo cha kawaida au naweza sema cha kienyeji” alisema Daqarro.

Alisema kuwa watanzania tunauwezo wa kuzalisha mazao bora kwakuwa tuna aridhi nzuri, maji mengi ya kutosha tunayo kwani tunamito mingi inayotoa maji hivyo tukiamua kuwekeza na kulima kilimo chakisasa tunaweza kusaidika na hata pato la mkulima litakuwa na sio mkulima tu na pia pato la serikali pia litaongezeka kutokana na kilimo.

Aidha mkuu huyo wilaya alisema kuwa serikali inawashukuru wadau kwa kuupa mkoa wa Arusha heshima ya kufanyika kwa maonyesho hayo ambayo yatafanyika kwa muda wa siku mbili hivyo amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi katika kujifunza teknolojia mpya za kilimo na ubunifu wautaalamu mbalimbali.
“Napenda pia kuwataka waonyeshaji kuangalia suala la bei kwani asilimia 75-80 ya wakulima ni wakulima wadogo wadogo hivyo ni vyema wakauza bidhaa zao kwa bei nafuu ili wakulima wa hali ya chini aweze kumudu kununua bidhaa ili waweze kuendana na kasi ya kilimo cha kisasa, Serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo wanaangalia ni kwa namna gani wataweza kuboresha sekta hii ya kilimo kwa kutoa elimu mbalimbali kwa wakulima ili kuepukana na kilimo duni ambacho kinasababisha hasara kwa wakulima nchini” alisema Daqorro

Kwa upande wake mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Seliani Dr Daniel Mafuru amesema kuwa wamekua wakishirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo, katika uzalishaji wa Teknolojia, pamoja na kuwatafutia wadau wa kilimo masoko ya mazao yao.

Aidha alisema kuwa Seliani wapo tayari kuwaunganisha wakulima na waonyeshaji wa teknologi, ilikuwawezesha wakulima kupata mafunzo na kubadilishana ujuzi pia iwapo watawaunganisha itawasaidia kufahamu namna ya kuhifadhi mazao yao baada ya uvunaji ili wasipoteze mazao kama ilivyokuwa kabla ya kupata elimu hiyo ya kilimo.

Kwa meneja masoko wa kampuni ya John Deere ambaye pia ndio wadhamini wakuu wa maonyesho haya Wayne Travas alisema kuwa kampuni yao zinafanya kazi ya kuwaletea wakulima wadogo mashine za kilimo ambazo zitawasaidia kufanya kazi vizuri na kwa teknologia za kisasa pamoja na ubora mwingi.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top