WEMA SEPETU ARUDI KWA KISHINDO INSTAGRAM

Baada ya takriban wiki 4 kupita kwa mwanadada Wema Sepetu kutoweka post yoyote katika page yake ya Instagram, hatimaye mrembo huyo amerudi tena kwa kishindo.
Wema Sepetu
Hiyo ni baada ya kufuta post zote katika page yake hiyo December 31 mwaka jana na kuamua kuuanza mwaka huu mpya kwa style hiyo iliyowashangaza wengi.

Ilipotimia saa 6 kamili za usiku wa kuamkia leo mwanadada Wema Sepetu aliamua kupost post yake ya kwanza kwa mwaka huu na kuwaomba wote ambao walim-miss wagonge like kama kishindo cha kurejea kwake.

Post hiyo ya kwanza ya Wema Sepetu ilijumuika na ahadi kwa mashabiki zake kwamba amewaandalia vitu vingi vizuri kwa mwaka huu wa 2017 na njia pekee ya kuvifahamu vitu hivyo ni kuendelea kubaki karibu naye katika page zake za mitandao ya kijamii.

Wema Sepetu

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post