Unknown Unknown Author
Title: MKUU WA WILAYA YA KILWA AMUAGIZA MKURUGENZI AMSIMAMISHE KAZI MGANGA MKUU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi, Christopher Ngubiagai akiongea na Waandishi wa Habari. Na. Ahmad Mmow. Kilwa. Mkuu wa wilay...
Christopher Ngubiagai
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi, Christopher Ngubiagai akiongea na Waandishi wa Habari.

Na. Ahmad Mmow. Kilwa.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi, Christopher Ngubiagai amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa, amsimamishe kazi mganga mkuu wa hospitali ya wilaya hiyo, Vitalis Katalyeba ilikupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili katika utendaji wake.

Ngubiagai alitoa agizo hilo jana akiwa katika kituo cha afya cha Tingi alipopitia kuangalia utekelezaji wa agizo lake kwa shirika la umeme (TANESCO) la kushugulikia changamoto ya umeme katika kituo hicho.

Ngubiagai alimtaka mkurugenzi amsimamishe Dr Katalyeba sambamba na kuunda tume itakayo mshirikisha mganga mkuu wa mkoa ili kuchunguza ukweli wa tuhuma na malalamiko yanayotolewa dhidi ya mtaalamu huyo.

Mkuu huyo wa wilaya ambae alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi na watumishi wa kituo hicho, alisema tuhuma anazotuhumiwa nazo hazivumiliki.

Hivyo kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sheria za utumishi na utawala bora anamtaka mkurugenzi amuweke pembeni ili uchunguzi upite.
"Natambua madaktari na wauguzi wanazo taratibu zao na mara zote huwa hawataki waingiliwe, lakini katika hili ni vigumu kuvumilia. Maana umuhimu na thamani yao ni kwasababu ya kuwahudumia wananchi lakini kama mtu anashindwa kufanya hivyo inakuwaje asiambiwe au kuwajibika," alihoji Ngubiagai.

Sambamba na kumuagiza mkurugenzi achukue hatua hiyo, pia amemuomba mganga mkuu wa mkoa wa Lindi kwa nafasi yake na kwakuzingatia taratibu, kanuni na sheria achunguze na kujiridhisha na kisha achukue hatua stahiki kwa Katalyeba iwapo mambo anayotuhumiwa na anayolalamikiwa ni yakweli.
"Huyo anazijua taratibu zao, achunguze na atueleze kama mambo yanayofanywa na daktari huyu ni sawa na taaluma yake, na majibu ya uchunguzi tunayataka," akisema. 

Ngubiagai aliyataja baadhi ya mambo yanayotakiwa kupatiwa majibu kwanini amewahamisha watumishi watano wa kituo hicho kwa mkupuo. Ikiwa ni muda mfupi tu tangu baadhi ya watumishi kueleza tatizo la umeme lililokuwa linasababisha nyakati fulani wajawazito kujifungulia kwa kutumia mwanga wa tochi, kuwanyanyasa baadhi watumishi waidara hiyo, na kubwa kuliko yote ni sababu ya kifo cha mwanafunzi wa darasa la pili wa shule ya msingi Miteja aliyefia katika kituo hicho baada ya kuchelewa kukimbizwa katika hospitali ya wilaya.

Ikielezwa kuwa mganga mkuu huyo hakutoa ushirikiano na muuguzi wa kituo hicho. Badala yake alimdharahu na kumueleza kuwa hakustahili kujulishwa na yeye. Hivyo alipeleka gari saa 10 alasiri wakati mtoto huyo akiwa amefariki. Japo kuwa taarifa hizo alipewa saa nne asubuhi. 

Awali mmoja wa wauguzi wa kituo hicho, Mwanaisha Amanzi, pamoja na kumshukuru mkuu huyo wa wilaya kutokana kumalizika kwa changamoto ya umeme katika kituo hicho lakini kitendo chake cha kumueleza tatizo hilo limemjengea uadui na mkuu wake wa idara.

Kwa sababu analaumiwa kwa kueleza tatizo hilo kwake na mbele ya waandishi wa habari.
"DC mimi na sakamwa hata nilipo muomba gari kwa ajili yule mwanafunzi aliyefariki hakunipa ushirikiano, aliishia kuniita kwa jina langu, Amanzi, Amanzi, Amanzi, Tingi mnamatatizo sana, kwani huyo mgonjwa anaumri gani, nilipomtajia anamiaka tisa akaniambia aliestahili kumpa taarifa hiyo sio mimi bali muuguzi wa zahanati ya Miteja. Alikata simu na hata nilipompigia tena alikuwa hapokei hadi nilipo tumia simu ya mtu mwingine nakumueleza huyo mgonjwa amefariki kwahiyo kama ataleta gari ni kwaajili ya kusafirisha maiti," alisema Mwanaisha.

Mlezi wa mtoto aliyefariki (Matilda Pinda, miaka tisa), Magreth Nguli aliunga mkono maelezo ya Mwanaisha kuhusu mazingira ya kifo cha mtoto Matilda.
"Kila alichokuwa anafanya huyo muuguzi na majibu ya huyo daktari tulikuwa tunasikia, hata alipoacha kupokea simu yake tulikuwa tunaona na ndipo tulimpa simu nyingine alipompigia alipokea, huenda alidharau kwakuwa aliyekuwa anaumwa ni mtoto. Kwasababu alipotajiwa umri wa mgonjwa alikata simu kabisa," alisema Magreth.

Mganga mfawidhi wa Kituo hicho, Christopher Kunde alikiri kuwa watumishi watano wa kituo hicho akiwamo Mwanaisha wamepata barua za uhamisho. Alisema ingawa barua hizo zimeeleza ni uhamisho wa kawaida lakini alishangaa kuona wanahamishwa wengi kwa mpigo. Tena ni muda mfupi tu baada ya kuibuliwa tatizo la umeme na maji katika kituo hicho.

Kwa upande wake, mganga mkuu huyo, Dr Katalyeba alipoulizwa kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hii kuhusu tuhuma na malalamiko hayo alisema yeye sio msemaji wa halmashauri ya wilaya. Hivyo aulizwe yeye kwasababu utaratibu, kanuni na sheria inataka hivyo. Na yeye anaheshimu mambo hayo.

Hata alipoambiwa na kukumbushwa tuhuma nyingi zinamlenga yeye binafsi, mganga Dkt Katalyeba alishikilia msimamo wake wakumtaka mwandishi awasiliane na DED wa Kilwa. Juhudi za kumpata DED wa Kilwa, Zabron Bugingo hazikuweza kufanikiwa baada ya simu yake kutokuwa hewani.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top